Naibu Waziri wa Afya Dkt. Mollel awasimamisha kazi DMO, Mfamasia na Mtunza stoo Ngara

Naibu Waziri wa Afya Dkt. Mollel awasimamisha kazi DMO, Mfamasia na Mtunza stoo Ngara

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk.Godwin Mollel, amewasimamisha kazi DMO, Mfamasia na Mtunza Stoo wa Hospitali ya Wilaya ya Ngara ya Nyamiaga mkoani Kagera ili kupisha uchuguzi. Watumishi hao wanakabiliwa na tuhuma za kuhusika na upotevu wa dawa za mamilioni ya fedha zilizoletwa na Serikali kwa ajili ya wananchi.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk.Godwin Mollel, amewasimamisha kazi DMO, Mfamasia na Mtunza Stoo wa Hospitali ya Wilaya ya Ngara ya Nyamiaga mkoani Kagera ili kupisha uchuguzi.

Watumishi hao wanakabiliwa na tuhuma za kuhusika na upotevu wa dawa za mamilioni ya fedha zilizoletwa na Serikali kwa ajili ya wananchi.

Akizungumza na Watumishi wa Afya wilayani humo juzi, Dk. Mollel amesema Serikali chini ya Rais Dk. John Magufuli, haiwezi kuvumilia watumishi wasio waadilifu wanaoiibia serikali kwa manufaa yao binafsi hivyo ni lazima wakae pembeni kwanza wakati uchunguzi wa tuhuma zao ukiendelea na itakapobainika wamehusika hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo (DMO), Revocatus Ndyekubora, Mfamasia wa Hospitali, Patrick Ogo na Mtunza Stoo, Gaston Bakulu, kwa tuhuma za kujihusha na utoroshaji wa dawa ya hospitali na kuziuza kwa wafanyabiashara.

Amesema watumishi hao wamekuwa wakishiriki kuihujumu serikali huku hosipitali, vituo vya afya na zahanati vikikosa madawa na wagonjwa kuhangaika kupata huduma wanapoenda kutibiwa.

Aidha, amemwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Aidan Bahama, kuwatafutia kazi nyingine watumishi.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »