Juma Mwambusi arejea kukinoa Kikosi cha Yanga

Juma Mwambusi arejea kukinoa Kikosi cha Yanga

Uongozi wa klabu ya Yanga umefanya mazungumzo na aliyekuwa Kocha msaidizi wa kikosi hicho Juma Mwambusi ili kuja kukinoa kikosi cha Klabu hiyo. Hatua hiyo inakuja baada ya klabu hiyo kutangza kuvunja mkataba na aliyekuwa kocha Mkuu, Cedric Kaze mnamo March 07, 2021.Juma Mwambusi aliomba kuvunja mkataba wake na yanga hivi karibuni kwa madai ya

Uongozi wa klabu ya Yanga umefanya mazungumzo na aliyekuwa Kocha msaidizi wa kikosi hicho Juma Mwambusi ili kuja kukinoa kikosi cha Klabu hiyo. Hatua hiyo inakuja baada ya klabu hiyo kutangza kuvunja mkataba na aliyekuwa kocha Mkuu, Cedric Kaze mnamo March 07, 2021.
Juma Mwambusi aliomba kuvunja mkataba wake na yanga hivi karibuni kwa madai ya kuumwa lakini sasa yuko sawa kiafya na anaweza kurejea kukinoa kikosi hicho cha yanga

Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Dkt. Mshindo Msola amesema ” Mwambusi ataichukua timu kwa sasa wakati tunamtafuta Mwalimu mwingine, na kwa bahati nzuri Mwambusi aliondoka na kuaga vizuri, na klabu ilimsaidia kupata matibabau wakati anaumwa na tokea ligi inaanza tulikuwa naye hivyo sio kwamba ana ugeni na timu”

Dkt. Msindo Msola ameyasema hayo akiwa anamtangaza Juma Mwambusi kuwa Kocha wa Yanga kwa muda.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »