Serikali iwekeze zaidi katika kutoa elimu juu ya namna ya kupambana na upungufu wa vitamini kwa njia nyepesi

Serikali iwekeze zaidi katika kutoa elimu juu ya namna ya kupambana na upungufu wa vitamini kwa njia nyepesi

Na Barnabas kisengi Mpwapwa March  10  2021 Vitamin A ni vitamin muhimu sana kiafya. Hii ni vitamin ambayo husaidia katika ujenzi wa tishu laini (kwenye misuli, kani na viungo vya ndani), tishu ngumu za mifupa na tishu zinazounda viwambo vya njia zinazohifadhi belaghami (mucas). Aidha afisa Lishe asunta amesema  vitamin A husaidia retina ya jicho kuzalisha

Na Barnabas kisengi Mpwapwa March  10  2021


Vitamin A ni vitamin muhimu sana kiafya. Hii ni vitamin ambayo husaidia katika ujenzi wa tishu laini (kwenye misuli, kani na viungo vya ndani), tishu ngumu za mifupa na tishu zinazounda viwambo vya njia zinazohifadhi belaghami (mucas).

Aidha afisa Lishe asunta amesema  vitamin A husaidia retina ya jicho kuzalisha viambata muhimu ambavyo ni vizuia vioksidishaji (antioxidants) muhimu vinavyohitajika kulinda jicho dhidi ya uharibifu unaweza kusababishwa na mwanga.


Sehemu kubwa ya uoni hafifu ambao unawakabili watu wengi hutokana na upungufu wa vitamin A.


“Utafiti uliofanyika nchini Tanzania mwaka 2010 na kupewa jina la Tanzania Demographic and Health Survey (TDHS) ulibaini kwamba kiasi cha 33% ya watoto wote chini ya umri wa miaka 5 walikuwa na upungufu wa vitamin A; na kiasi cha 37% ya kina mama wenye umri wa kati ya miaka15 – 49 walikuwa na upungufu pia.”amesema asunta


Matokeo haya yaliisaidia serikali, kwa msaada wa wahisani, kuanzisha kampeni kubwa ya kutoa (hususan kwa watoto) vitamin A kama kiinilishe cha ziada.
Aidha matokeo ya utafiti huu pia yalizaa wazo la kuongeza vitamin A kwenye baadhi ya vyakula (hususan unga wa mahindi na ngano),  kama njia nyepesi ya kupambana na upungufu.


“Hatua hizi za serikali ni njema na bila shaka zinastahili pongezi nyingi. Pamoja na pongezi hizi kuna haja kwa serikali kuanzisha pia kampeni kubwa, inayolenga kutoa elimu ya kina kwa wananchi juu ya tatizo la upungufu wa vitamin A, na njia bora za kuipata bila kusubiri msaada wa serikali.”alifafanua asunta

Elimu hii ielekeze ni vyakula gani ambavyo wananchi wakivitumia katika mazingira yao watakwepa kuwa na upungufu wa vitamin A. 


Kwa mfano karoti. Matumizi ya karoti kila siku, iwe kwa kutafuna au katika mfumo wa juisi, yanaweza kuwa msaada mkubwa kwa mtu mwenye upungufu vitamin A.
Viazi lishe (orange fleshed sweet potatoes) ni chanzo kingine kikubwa sana cha vitamin A. Matumizi mapana ya  viazi lishe yanaweza kuwa suluhisho la kudumu la upungufu wa vitamin A nchini.


Tatizo ni kwamba watu wenye uelewa juu ya viazi lishe ni wachache sana. Serikali inaweza ikatatua hili kwa kutoa elimu zaidi na kusambaza mbegu katika halmashauri zote nchini. 

Ilivyo hivi sasa ni kwamba viazi lishe ni moja ya mazao ambayo watu wanaanza kuyalima kibiashara. Ziko kampuni mbili tatu ambazo zinanunua viazi lishe kwa ajili ya kusafirisha nje ya nchi. 


Katika masoko ya ndani, kwa mfano soko kuu la Kariakoo, viazi lishe vina bei nzuri sana ukilinganisha na viazi vya kawaida. Hivi sasa sokoni Kariakoo kilo ya viazi lishe ni shilingi 4,000.00, wakati ile ya viazi vitamu vya kawaida ni shilingi kati ya 1500.00 – 2000.00.


Serikali pia inaweza kuhamasisha matumizi makubwa ya mlonge. Mlonge ni zao lenye kiasi kikubwa cha viini lishe tofauti tofauti . Wenzetu waliotuzidi maarifa huko nje ya nchi wameuingiza mlonge katika kundi la vile vyakula wanavyoviita ‘superfoods’.

Matumizi ya mlonge yanaweza kutatua tatizo la utapiamlo kwa mapana na marefu. Kwa mfano, katika suala la vitamin A, gramu kwa gramu, unga wa majani ya mlonge una vitamin A mara kumi zaidi kuliko karoti!


Mlonge siyo zao gumu kulipanda na kulikuza. Ni zao lenye uwezo wa kuhimili takriban hali za hewa za aina zote. Serikali itakuwa imefanya jambo kubwa sana iwapo itahimiza matumizi mapana ya mlonge hapa nchini.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »