Halmashauri ya Mji wa Makambako yapewa siku 30 kuboresha upatikanaji wa dawa.

Halmashauri ya Mji wa Makambako yapewa siku 30 kuboresha upatikanaji wa dawa.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Festo Dugange ametoa muda wa siku thelathini kwa Uongozi wa Halmashauri ya Mji wa Makambako Mkoani Njombe kuhakikisha unafanya ukaguzi wa manunuzi na matumizi ya Dawa katika Kituo cha Afya cha Mji huo kwa kipindi cha miezi sita iliyopita ili kujiridhisha na malalamiko ya Wananchi ya ukosefu wa

Inaweza kuwa picha ya Watu 4, watu wanasimama, watu wanakaa na ndani

Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Festo Dugange ametoa muda wa siku thelathini kwa Uongozi wa Halmashauri ya Mji wa Makambako Mkoani Njombe kuhakikisha unafanya ukaguzi wa manunuzi na matumizi ya Dawa katika Kituo cha Afya cha Mji huo kwa kipindi cha miezi sita iliyopita ili kujiridhisha na malalamiko ya Wananchi ya ukosefu wa Dawa.

Ametoa maagizo hayo Machi 09,2021 wakati wa ziara yake ya Kikazi ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya katika Halmashauri ya Mji wa Makambako ambapo alibaini kuwa upatikanaji wa dawa katika kituo hicho ni asilimia 30 badala ya asilimia 95 mujibu wa mwongozo wa Serikali.

“Baada ya siku thelathini nilizoagiza nikiona hakuna kilichofanyika nitachukua hatua kali za Kisheria kwa mujibu wa sheria kwa hiyo Mkurugenzi na Mganga Mkuu hakikisheni mnasimamia hili kwa wakati,” amesema Dkt, Dugange.

Amesema upungufu huo mesababisha kushuka kwa mapato ya Hospital hiyo ambayo imekuwa ikikusanya wastani wa Shilingi laki tatu kwa siku tofauti na wingi wa Watu wa Mji huo hali inayopelekea Wagonjwa kukosa Dawa na kupata huduma zisizoridhisha, hivyo kuibua malalamiko miongoni mwa Wananchi wanaopata huduma kwenye Kituo hicho.

“Haiwezekani kila Mgonjwa anaekuja kutibiwa hapa awe na Msamaha hapana hii haikubaliki baadhi ya Watumishi wetu wanatumia vibaya misamaha yaani wanaweka Fedha mfukoni halafu wanaandika ametibiwa kwa msamaha,” ameongeza Dkt. Dugange.

Awali Mbunge wa Jimbo la Makambako Mhe Deo Sanga alimweleza Dkt Dugange kuwa kituo hicho kina umuhimu mkubwa kwa kuwa kinahudumia jamii ya Wakazi wa Makambako na maeneo ya jirani ya Mikoa wa Iringa na Morogoro.

“Mhe, Naibu Waziri Kituo hiki kinahudumia Wananchi wengi wengine wanatoka maeneo ya Mikoa jirani ya Morogoro na Iringa hivyo naungana na wewe kuwa Watumishi wetu lazima wawe waaminifu ili Kituo hiki kiendelee kuboreshwa kila siku” ameeleza Mhe Sanga.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Njombe Mhe Ruth Msafiri ameahidi kusimamia utekelezaji wa maelekezo yaliyotolewa na Naibu Waziri ndani ya muda husika uliopangwa na kuwasilisha ripoti ya utekelezaji

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »