UKATILI WA KIUCHUMI KIKWAZO CHA HARAKATI ZA WANAWAKE KATIKA UONGOZI

UKATILI WA KIUCHUMI KIKWAZO CHA HARAKATI ZA WANAWAKE KATIKA UONGOZI

Na Barnabas Kisengi-KongwaMachi 15, 2021 Ukatili kiuchumi wakwamisha harakati za Wanawake kushiriki katika masuala ya Uongozi Wilayani kongwa Mkoani Dodoma. Wameyasema hayo wanawake kwenye Mjadala kongamano  katika muendelezo wa maadhimisho ya Siku ya wanawake duniani iliyoadhimishwa na Shirika la wanawake katika Sheria na maendeleo barani Afrika (WILDAF) kwa kushirikiana na wanawake mbalimbali Wilayani kongwa Machi

Na Barnabas Kisengi-Kongwa
Machi 15, 2021


Ukatili kiuchumi wakwamisha harakati za Wanawake kushiriki katika masuala ya Uongozi Wilayani kongwa Mkoani Dodoma.


Wameyasema hayo wanawake kwenye Mjadala kongamano  katika muendelezo wa maadhimisho ya Siku ya wanawake duniani iliyoadhimishwa na Shirika la wanawake katika Sheria na maendeleo barani Afrika (WILDAF) kwa kushirikiana na wanawake mbalimbali Wilayani kongwa Machi 13 2021.


Bi Neema Mayunga mfanyakakazi kutoka shirika la WILDAF akisoma risala mbele ya mgeni Rasmi, Katibu Tarafa wa tarafa ya Kongwa Bw.Denis Semindu aliyemwakilisha mkuu wa Wilaya ya kongwa amesema mwezi huu ni muhimu katika kufanya muendelezo wa Sikukuu ya wanawake kwani unatoa fursa kwa mwanamke na jamii katika kujadili changamoto na fursa zinazomzunguka mwanamke hususani masuala ya uongozi.


Naye Mkuu wa kitengo cha kijinsia Halmashauri ya Kongwa Bi Faraja Kasuwi amesema Shirika la WILDAF linatekeleza mradi wa “Mwanamke Sasa” ambao huwajengea uwezo wanawake katika Sheria na Uongozi unaotekelezwa katika Kata Saba Wilayani humo ambazo ni Hogoro, Mkoka, Matongoro, Mtanana, Kibaigwa, Lenjulu na Kongwa.

Bi Kasuwi kwa Niaba ya mkulugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya kongwa kwa  kupitia idara ya maendeleo ya Jamii ametoa shukrani kfwa mradi huo kwa kutambua ustawi wa Mwanamke wa Kongwa kwa kuwajengea uwezo kuhusu masuala ya uongozi na kupinga Ukatili Kijinsia.
Aidha Bi Kasuwi amesema mradi huo unashirikisha makundi mbalimbali wakiwemo mama Lishe, bodaboda, watu maarufu, viongozi wa Dini,wazee wa kimila, viongozi wa kata,watendaji wa vijiji,wasaidizi wa kisheria(Paralegal) na Mabaraza ya migogoro kwenye Kata.


Akisoma Hotuba ya Mgeni Rasmi kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya, Katibu Tarafa,  Bw.Semindu amesema  ili wanawake kufikia usawa  Serikali, Jamii na mashirika mbalimbali Hazina Budi kuchukua juhudi kujikwamua zikiwemo wanawake kujitambua, kuchangamkia fursa,kugombea nafasi mbalimbali katika Uongozi, kumlinda mtoto wa kike na  mimba na ndoa za utotoni pamoja na wanawake  kushiriki katika shughuli za uzalishaji.


Kwa upande wake Diwani viti maalumu Mh. Monica Nyabu akichangia maoni katika mjadala wa kongamano hilo maswali na majibu  yaliyoshirikisha wanawake wote  na WILDAF katika shughuli hiyo amesema,Faida kubwa ya Mwanamke kuwa kiongozi ni kumuwezesha kushiriki katika maamuzi ya Jamii anayoiongoza, pia kuna shida zingine za Wanawake ni lazima wakutane na kiongozi wa kike ndio huwa huru kuzungumziwa.
WILDAF waliainisha Changamoto za rushwa hususani rushwa ya ngono,kukosekana kwa utashi wa kisiasa katika vyama vya siasa, wanawake kukosa fursa za elimu,fikra potofu na mitazamo hasi iliyojengeka katika Jamii kuwa Uongozi wa kisiasa ni nafasi za wanaume Baadhi ya watu wanaamini kuwa ndizo huwafanya wanawake washindwe kujihusisha na Uongozi.


Katika Mjadala huo wanawake wengi walisema pamoja na changamoto nyingi lakini kubwa inayowafanya wanawake wasifanikiwe kuwa viongozi ni Ukatili wa kiuchumi, Ambapo wakati wa uchaguzi Mwanamke anaweza kukosa kutumia hata rasilimali walizochuma na mwanaume kumsaidia katika uchaguzi, na Jamii kwa sehemu kubwa bado inatafsiri bila fedha huwezi kuwa kiongozi bora.


Kaulimbiu : “Wanawake katika uongozi chachu kufikia Dunia yenye usawa”

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »