Kilimanjaro kujenga uwanja wa mpira wa Kikapu

Kilimanjaro kujenga uwanja wa mpira wa Kikapu

Mkoa wa Kilimanjaro uko mbioni kuanza ujenzi wa uwanja wa mpya wa kikapu ambao utakuwa wa umma. Mkoa huo hadi sasa hauna kiwanja chochote cha umma, na wachezaji wa kikapu wanategemea viwanja vya taasisi binafsi na baadhi ya shule chache zenye viwanja. Katika mazungumzo yaliyofanyika kati ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mghwira na

Mkoa wa Kilimanjaro uko mbioni kuanza ujenzi wa uwanja wa mpya wa kikapu ambao utakuwa wa umma.

Mkoa huo hadi sasa hauna kiwanja chochote cha umma, na wachezaji wa kikapu wanategemea viwanja vya taasisi binafsi na baadhi ya shule chache zenye viwanja.

Katika mazungumzo yaliyofanyika kati ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mghwira na Rais wa Shirikisho la mpira wa kikapu Tanzania Ndg. Phares Magesa, walikubaliana kuwa Serikali ya Mkoa itaendelea kushirikiana na Chama cha Mpira wa kikapu Kilimanjaro ili kufanikisha shughuli za kikapu na kuhakikisha mkoa wa Kilimanjaro unakuwa na uwanja wake ambao utakuwa wa umma ili kutoa fursa kwa vijana wengi zaidi kucheza kikapu, uwanja huo utasaidia vijana walioko mitaani na wanafunzi wa shule za sekondari na za msingi ambazo nyingi hazina viwanja vya Kikapu.

Rais wa TBF Ndg. Magesa alipata nafasi ya kuongea na Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mhe. Rajab Kundya, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa Ndg. Msangila, Meya wa Manispaa ya Moshi Mstahiki Juma na Mkurugenzi wa Manispaa ambao wote walimhakikishia ushirikiano wa hali ya juu katika kuendeleza mchezo wa kikapu mkoani Kilimanjaro na kufanya kila linalowezekana uwanja wa kikapu ujengwe kwa kuanzia Manispaa ya Moshi na baadae kila Halmashauri na pia mashuleni.

Rais wa TBF Ndg. Magesa aliwashukuru Viongozi wote wa mkoa wa Kilimanjaro kwa ushirikiano wanaotoa kuendeleza mchezo wa kikapu na kuwataka kufuatilia ili ahadi hiyo itimie ndani ya muda mfupi ujao, katika mikutano hiyo pia walihudhuria Afisa Michezo wa mkoa Ndg. Ishumi na Mwenyekiti wa Chama cha mpira wa kikapu Kilimanjaro Ndg. John Mmbando.

Katika ziara ya mkoa wa Kilimanjaro Rais wa TBF pia alitembelea maeneo yanayotarajiwa kujengwa viwanja vya Kikapu vya umma na pia alitembelea baadhi ya taasisi zenye viwanja vya Kikapu na kuomba taasisi hizo ziendelee kuruhusu vijana wengi waweze kutumia viwanja hivyo.
Taasisi ya Rafiki Foundation ina uwanja mzuri wa ndani na wa nje na Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Ndg. Phil Nickel amemueleza Rais wa Shirikisho la mpira wa kikapu Tanzania Ndg. Phares Magesa kuwa taasisi hiyo iko tayari kutoa viwanja vyake vitumike kwa ajili ya wachezaji wa kikapu wa nje ya shule yao, na pia kutumia kwa mafunzo maalumu, kambi za timu na mashindano mbalimbali kulingana na mahitaji ili mradi haitaingiliana na masomo yao.

Taasisi ya Don Bosco ya Moshi pia ina uwanja wa nje ambapo Mkurugenzi wa Don Bosco pia alimueleza Rais wa TBF kuwa wao wanaruhusu vijana wa nje ya taasisi zao kutumia uwanja wao, Rais wa TBF na ujumbe wake walishauri Don Bosco ifikirie kuboresha uwanja wake kwa kuweka taa ili uweze kuchezewa hata usiku.

Katika ziara hiyo Rais wa TBF alipata pia nafasi ya kuongea na wazazi, walimu, wachezaji wakubwa na watoto wa shule za msingi hadi sekondari ambao alikutana nao katika viwanja na shule mbalimbali alizotembelea, aliwaasa wanafunzi wacheze kikapu, wazingatie masomo na wawe na nidhamu ili waweze kufanikiwa na pia aliwaasa wazazi na walezi waruhusu watoto wacheze michezo hususani kikapu na kuwasaidia vifaa wanapohitaji.
Aidha Rais wa TBF aliwataka walimu wote mashuleni wawape fursa vijana ya kucheza michezo hususani kikapu wakati wa vipindi vya michezo na shule ambazo hazina viwanja zifanye utaratibu wa kutumia viwanja vya shule jirani sambamba na kufanya jitihada za kuwa na viwanja vyao vya kikapu, pia Rais wa TBF aliwaasa walimu na wachezaji wa zamani wachangamkie fursa za kujifunza ualimu au uamuzi wa mchezo wa kikapu kila fursa inapopatikana ili waweze kujiongezea vipato na kusaidia kuendeleza mchezo kiufundi zaidi.

Rais wa TBF pia alipata nafasi ya kuongea na wadau kadhaa ikiwa ni pamoja na taasisi za kifedha, wafanyakazi na wafanyabiashara ambao wameahidi kuchangia ujenzi wa uwanja mpya wa kikapu katika manispaa ya Moshi na ameahidi kurudi mkoani Kilimanjaro ndani ya miezi mitatu ijayo ili kuja kufungua uwanja mpya wa kikapu ambao utakuwa umejengwa.

Rais wa TBF ataendelea na ziara ya kuhamasisha wadau kujitokeza kufadhili na kuwekeza katika mchezo wa kikapu na ikiwa ni pamoja na kujenga viwanja vya Kikapu mikoa yote nchini Tanzania.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »