KUPUNGUA VIFO VYA MAMA NA MTOTO WILAYA YA KILOMBERO.

KUPUNGUA VIFO VYA MAMA NA MTOTO WILAYA YA KILOMBERO.

NA MWANDISHI WETU, MOROGORO IDADI ya vifonvya akinamama na watoto wilayani Kilombero imetajwa kupungua kwa zaidi ya asilimia 80 katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita kutokana na utekelzaji wa mradi wa huduma mkoba wa cliniki inayotembea unaotekelwaza na shirika lisilo la kiserikli Plan International Tanzania. Hayo yalibainishwa jana na Mratibu wa chanjo wa Halmashauri ya

NA MWANDISHI WETU, MOROGORO

IDADI ya vifonvya akinamama na watoto wilayani Kilombero imetajwa kupungua kwa zaidi ya asilimia 80 katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita kutokana na utekelzaji wa mradi wa huduma mkoba wa cliniki inayotembea unaotekelwaza na shirika lisilo la kiserikli Plan International Tanzania.

Hayo yalibainishwa jana na Mratibu wa chanjo wa Halmashauri ya Mlimba, Nendaheli Malugu wakati wa ziara ya pamoja kati ya viongozi wa Serikali na shirika la Plan International katika kutathimini maendeleo ya mradi huo wa gari maalum la wagonjwa na pikipiki 18 zilizokuwa zimetolew kwa wahudumu wa afya.

Alisema licha ya halmashauri ya Mlimba kukabiliwa na upungufu wa zahanati zaidi ya asilimia  67 na uwepo wa vituo vya afya viwili katika kata 16 katika halmashauri hiyo,  mradi huo wa huduma mkoba umefika vijiji 117 ambapo kati ya hivyo vituo 36 zinasaidiwa na plan kwakuwa ni vigumu kufikika kiraisi.

“kuanzishwa kwa huduma hii ya mkoba kumesaidia sana akina mama kutembea umbali mrefu katika kufuata huduma za chanjo ambampo wakati wa masika hulazimika kutumia gharama hadi 30,000 kufata huduma kwa pikipiki kwa umbali wa kilomita 40 ukizingatia  kwa chanjo zinazotakiwa kutolewa kila mwezi”. Alisema Malugu

Kadhalika alilishukuru shirika la Plan International kwa ufadhiri huo kwani kabla ya ufadhiri huo changamoto za akina mama zilikuwa nyingi zikiwemo baadhi kulazimika kuzalia nyumbani au barabarani kutokana na kuchelewa kufika katika vituo kwa wakati kwa sababu ya umbali uliopo.

Kwa upande wake Mkurugunzi wa miradi toka shirika la Plan International Peter Mwakabale alisema kuwa mradi huo ulianza kutekelezwa miaka 3 iliyopita na unatarajia kumalizika mwezi juni mwaka huu 2021.

Alifafanua mradi huo wa Kliniki inayotembea umelenga kumfuata mama aliko na kutoa chanjo ya uzazi wa mpango, upimaji wa mama mjamzito na kuwasaidia watoto humua ya afya ambapo mara baada ya kukamilikamradi huo shirika Litaendela  mkono jitihada zote za nguvu za wananchi na serikali katika uanzishwaji wa ujenzi wa vituo vya afya na zahanati ktk maeneo yao kwa kugharamia vifaa vyote vya viwandani.

“mradi huu umeleta mafanikiomakubwa katika kupunguza vifo vya akina mama na watoto lakini sasa unaelekea ukingoni mwazi junisisikama shirika tutaendelea kushirikiana na wananchi na serikali katika ujenzi wa zahanati mpya nakwa kuanza tayari tumeshatoa mifuko ya 260 saruji, nondona kilo 25 za misumari ilikusaidiaujezi wa zahanati ya kijiji cha Mkuyuni kata ya Chisano” alisema Mwakabale.

Mhandisi Stephano Kaliwa ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mlimba alieleza kuwa jitihada za Halmashauri katika kutekelza sara ya afya zinaendelea kuchukuliwa ikiwemo kuendelea na ujenzi wa hospitali ya Wilaya ambapo Serikali kuu ilishatoa milioni 500  kukamilisha ujenzi huo  ambao unatarajiwa kukamirika hivi karibuni na Hospitali kuanza kutoa huduma  ifikapo mwezi 4 mwaka huu.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »