Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Joseph Magufuli amefariki dunia. Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan kupitia Televisheni ya Taifa (TBC) leo usiku Machi 17, 2021 saa 5 usiku ametangaza kifo cha Rais Magufuli ambae amefariki dunia leo kwa maradhi ya Moyo akiwa katika Hospitali ya Mzena jijini Dar. Rais Magufuli alilazwa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Joseph Magufuli amefariki dunia.
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan kupitia Televisheni ya Taifa (TBC) leo usiku Machi 17, 2021 saa 5 usiku ametangaza kifo cha Rais Magufuli ambae amefariki dunia leo kwa maradhi ya Moyo akiwa katika Hospitali ya Mzena jijini Dar. Rais Magufuli alilazwa tarehe 6 Machi katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete kwa tatizo la moyo wa mfumo wa umeme.
Nchi itakuwa katika kipindi cha maombolezo kwa siku 14 na bendera zitapepea nusu mlingoti
Leave a Comment
Your email address will not be published. Required fields are marked with *