Mratibu wa Damu Salama jiji la Dodoma Jerome Malando amesema mahitaji ya Damu salama katika jiji la Dodoma ni chupa hamsini huku wito ukitolewa kwa kila mmoja kuguswa kuchangia damu salama ili kuokoa maisha ya watu. Malando amebainisha hay oleo Machi,20,2020 katika kanisa la Waadventista Wasabato Kikuyu jijini Dodoma wakati wa uchangiaji wa Damu Salama

Mratibu wa Damu Salama jiji la Dodoma Jerome Malando amesema mahitaji ya Damu salama katika jiji la Dodoma ni chupa hamsini huku wito ukitolewa kwa kila mmoja kuguswa kuchangia damu salama ili kuokoa maisha ya watu.
Malando amebainisha hay oleo Machi,20,2020 katika kanisa la Waadventista Wasabato Kikuyu jijini Dodoma wakati wa uchangiaji wa Damu Salama bure katika kuadhimisha Juma la Matendo ya Huruma kanisa la Waadventista Ulimwenguni.
Mratibu huyo wa Damu salama katika jiji la Dodoma amesema damu ina mahitaji makubwa katika uhai wa binadamu na haiwezi kuzalishwa katika kiwanda chochote hivyo ni muhimu kila mmoja kuguswa kuchangia damu ambapo jiji la Dodoma lina uhitaji wa chupa 50 za damu kila wiki.
Malando ametumia fursa hiyo kulipongeza kanisa la Waadventista Wasabato kwa kuwa na desturi ya kuadhimisha matendo ya huruma kwa kutoa misaada mbalimbali kwa jamii ikiwemo kuchangia damu huku Mzee wa kanisa la Waadventista Wasabato Kikuyu Elias Aron akielezea jinsi walivyoguswa katika utoaji wa damu salama .
Kwa upande wao baadhi ya washriki kwa Kanisa la Waadventista Wasabato Kikuyu akiwemo Samwel Makumil,Deus Mchoo,Victoria Mkama pamoja na Paula Kazima wamesema suala la uchangiaji wa Damu ni sehemu ya ibaada katika kuokoa watu wenye matatizo mbalimbali.
Na Barnabas kisengi Dodoma.
March 20 2021
Leave a Comment
Your email address will not be published. Required fields are marked with *