RAIS DK. MWINYI AMEONGOZA WANANCHI WA ZANZIBAR KUUAGA MWILI WA HAYATI DK. MAGUFULI (+VIDEO)

RAIS DK. MWINYI AMEONGOZA WANANCHI WA ZANZIBAR KUUAGA MWILI WA HAYATI DK. MAGUFULI (+VIDEO)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema kifo cha aliekuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli kimewacha simanzi na huzuni kubwa katika mioyo ya wananchi wa Tanzania na wapenda amani kote Barani Afrika. Dk. Mwinyi amesema hayo Uwanja wa Amani Jijini hapa, katika

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema kifo cha aliekuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli kimewacha simanzi na huzuni kubwa katika mioyo ya wananchi wa Tanzania na wapenda amani kote Barani Afrika.

Dk. Mwinyi amesema hayo Uwanja wa Amani Jijini hapa, katika hafla maalum ya kuuga mwili wa Hayati Dk. Magufuli, aliefariki dunia Machi 17, 2021.

Amesema kuhusiana na kifo hicho, Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na ile ya Zanzibar zimefanya juhudi kubwa  kuhakikisha Watanzania wengi  wanapata fursa ya kutoa heshima zao za mwisho na kuuaga mwili wa Kiongozi huyo.

Aliwapongeza wananchi  wa Zanzibar kwa kujitokeza kwa wingi katika hafla ya kutoa heshima na kuaga mwili wa Hayati Dk. Magufuli, sambamba akatoa pole kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan pamoja  na wana familia, huku akibainisha kuwa kifo hicho kimeleta simanzi na huzuni kubwa kwao kutokana na mapenzi makubwa walionayo kwa kiongozi wao.

Alieleza kuwa Watanzania wamepoteza kiongozi  mahiri na mwenye kipaji katika Bara la Afrika, mwenye kijipambanua na mtetezi wa haki za wanyonge, sambamba na mwenye azma ya kudumisha Muungano wa Tanzania.

Alisema Hayati Dk. John Pombe Magufuli alikuwa Kiongozi mwenye maono makubwa ya kuhakikisha Taifala Tanzania linapata maendeleo makubwa kupitia rasilimali zake.

Aidha alisema Hayati Dk. Magufuli atakumbukwa kwa kuendeleza miradi mikubwa ya maendeleo katika kipindi kifupi pamoja na kufanya juhudi ya kuhakikisha Tanzania inabaki kuwa salama na utulivu.

Alisema Watanzanaia watendelea kumkumbuka kiongozi huyo kwa kuwa mstari wa mbele katika kupigania haki za wanyonge,  aliepigania rasilimali za Taifa na kupinga rushwa pamoja na kusimamia uwajibikaji katika utumishi wa umma, huku akibainisha kuwa ameiwacha Tanzania ikiwa salama na amani na kuwa kigezo katika Afrika katika kila nyanja.

Rais Dk. Mwinyi alisema  Kiongozi huyo ni hidaya kutoka kwa Mungu, hivyo akasisitiza umuhimu wa kuendelea kuyaenzi na kuyadumisha yale aliyoyaacha pamoja na kumtegemea Mungu kwa kila jambo.

Aidha Dk. Mwinyi alisisitiza umuhimu wa Watanzania kuendelea kuwa wamoja na kushikamana katika kipindi hiki cha majonzi.

Alisema ni wajibu wa Watanzania wote kumomba Mungu ampe malazi mema kiongozi huyo pamoja na kubainisha azma ya Serikali anayoingoza ya kuendelea kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika kutumikia wadhalifa alionao, akibainisha uwezo mkubwa alionao kiongozi huyo-.

Alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itampa kiongozi huyo kila aina ya ushirikiano ili kufanikisha malengo yaliowekwa, ikiwemo yale aliyoyaacha Hayati Dk. Magufuli.

Mapema, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi aliongoza mapokezi ya mwili wa Hayati Dk. Magufuli, uliowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume majira ya saa 3.15 za asubuhi ukitokea Mkoani Dodoma kwa ndege ya shirika la Ndege la Air Tanzania, kabla msafara wake kufikishwa Uwanjwa  wa Amani kwa ajili ya kuagwa..

Nae, Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Majaliwa Kassim Majaliwa ambae Mwenyekiti wa Kamati ya Mazishi Kitaifa alisema Watanzania wanaendelea kupita katika kipindi cha huzuni kubwa, tangu kifo cha Rais Dk. John Pombe Magufuli kilipotokea Machi 17, 2021.

Alisema tukio la kuondokewa na Kiongozi mkuu wa Taifa  alioko madarakani sio jambo la kawaida, akibainisha limetokea kutokana na kudra za Mungu, hivyo akawataka Watanzania waipokeee hali hiyo mbali na marajio makubwa waliyonayo.

Alisema mkusanyiko  huo mkubwa wa wananchi ulioanzia Uwanja wa Ndege wa Abeid Amani Karume hadi Uwanja wa Amani unathibitisha huzuni waliyonayo wananchi  hao kwa  Kiongozi huyo.

Aidha, alisema mkusanyiko huo ni tukio linalotoa fursa kwa wananchi kupata nafasi ya kupita mbele ya Jeneza na kutoa heshima zao za mwisho kwa Marehemu.

Waziri Mkuu Mjaaliwa alitumia nafasi hiyo kutoa pole kwa Rais wa Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi,  Wananachi pamoja na wanafamilia wa Marehemu Mmagufuli kwa msiba huo mzito na kuwataka kuwa na subira katika kipindi hiki kigumu.

Katika hatua nyingine, Viongozi mbali mbali wa dini na madhehebu tofauti hapa Zanzibar, akiwemo Mhashamu Askofu Agostino Shao  kutoka Kanisa la Roman Katoliki,  Askofu Michael Hafidh kutoka Kanisa la Anglikan pamoja na Kiongozi wa Dini ya Kihindu waliomba dua ya kumtakia malazi mema Marehemu ,sambamba na Naibu Kadhi wa Zanzibar Sheikh Othman Hassan Ngwali, alieomba dua kama hiyo kwa upande wa dini ya Kiislamu .

Katika hafla hiyo Viongozi mbali mbali wa Kitaifa walishiriki, akiwemo Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Majaliwa Kasssim Majaliwa, Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla, Makamo wa Pili wa Rais mstaafu Balozi Seif Ali iddi, Mawaziri wa serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Zanzibar, Viongozi wa Vyama vya Siasa, Viongozi wa dini, Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama, Mabalozi wa Tanzania walioko nchi za nje, Mabalozi wan je nchini Tanzania, Wanafamilia pamoja na viongozi wengine.  

Postal Address: 2422 Tel.:0777476982. Fax: 024 2231822 

 E-mail: abdya062@gmail.com

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »