SERIKALI YATANGAZA TAHASUSI MPYA KWA KIDATO CHA TANO (+VIDEO)

SERIKALI YATANGAZA TAHASUSI MPYA KWA KIDATO CHA TANO (+VIDEO)

Taarifa muhimu kwa Wanafunzi waliomaliza Kidato cha Nne, mwaka 2020 Waziri Jafo ametangaza utaratibu wa wahitimu wa Kidato cha Nne mwaka 2020 kubadilisha Tahasusi(Combination) za Kidato cha Tano na Kozi za Vyuo vya Elimu ya Ufundi kwa njia ya mtandao kwenye mfumo wa Kieletroniki wa uchaguzi wa Kidato cha Tano na vyuo mwaka 2021. Amesema

Taarifa muhimu kwa Wanafunzi waliomaliza Kidato cha Nne, mwaka 2020

Waziri Jafo ametangaza utaratibu wa wahitimu wa Kidato cha Nne mwaka 2020 kubadilisha Tahasusi(Combination) za Kidato cha Tano na Kozi za Vyuo vya Elimu ya Ufundi kwa njia ya mtandao kwenye mfumo wa Kieletroniki wa uchaguzi wa Kidato cha Tano na vyuo mwaka 2021.

Amesema Waziri Jafo Zoezi hili litafanyika kuanzia tarehe 29/03/2021 hadi tarehe 11/04/2021 saa sita usiku. Hivyo, wanafunzi wanaotaka kufanya mabadiliko wanatakiwa kuingia kwenye mfumo wa uchaguzi wa wanafunzi unaopatikana katika anuani ya selform tamisemi

Mwisho ni kutangazwa kwa Tahasusi mpya zilizoanzishwa kwa wanafaunzi wa kidato cha Tano, mwaka 2021 kama ifuatavyo:-

  1. Physics, Mathematics, Computer studies (PMC) watasoma shule ya sekondari Dodoma ni wasichana na Shule ya sekondari ya ufundi Iyunga ni wavulana.
  2. Kiswahili, French, Chinese (KFC) watasoma sekondari ya Morogoro ni wasichana na wavulana watasoma sekondari ya Usagara.
  3. Kiswahili, English ,Chinese(KEC) watasoma sekondari ya Morogoro ni wasichana na wavulana watasoma sekondari ya Usagara.
  4. Physical Education,Biology, Fine Arts (PEBFA) watasoma wasichana shule ya sekondari Makambako na wavulana wao ni sekondari ya Kibiti. Pia, shule ya sekondari ya Mpwapwa ni kwa ajili ya wasichana na wavulana kwa tahasusi ya PEBFA.
  5. Physical Education, Geography,Economics (PEGE) watasoma wasichana shule ya sekondari Makambako na wavulana wao ni sekondari ya Kibiti. Pia, shule ya sekondari ya Mpwapwa ni kwa ajili ya wasichana na wavulana kwa tahasusi ya PEGE.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »