RAIS SAMIA AMPENDEKEZA DKT. MPANGO KUWA MAKAMU WA RAIS, BUNGE LAMPITISHA KWA 100% (+VIDEO)

RAIS SAMIA AMPENDEKEZA DKT. MPANGO KUWA MAKAMU WA RAIS, BUNGE LAMPITISHA KWA 100% (+VIDEO)

Jina hilo limepelekwa Bungeni na Mpambe wa Rais (ADC) Kanali Nyamburi Mashauri, na kukabidhiwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai. Mheshimiwa Spika, nawasilisha Bungeni Jina la Mheshimiwa Philip Isdori Mpango kwa Nafasi ya Makamu wa Rais Tanzania. Bunge lamthibitisha kwa kishindoBunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limemthibitisha Dkt. Philip

Jina hilo limepelekwa Bungeni na Mpambe wa Rais (ADC) Kanali Nyamburi Mashauri, na kukabidhiwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai.

Mheshimiwa Spika, nawasilisha Bungeni Jina la Mheshimiwa Philip Isdori Mpango kwa Nafasi ya Makamu wa Rais Tanzania.

Bunge lamthibitisha kwa kishindo
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limemthibitisha Dkt. Philip Isdor Mpango kwa asilimia 100 kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kura zote 363 za wabunge waliopiga kura.

​WASIFU WA DKT. PHILIP ISDOR MPANGO

Dk Philip Mpango alizaliwa July 14, 1957 alikuwa ni Waziri wa Fedha na Mipango katika Serikali ya Awamu ya Tano.

Mpango ni mzaliwa wa Kigoma, baba yake ni marehemu Isidori Nzabhayanga Mpango, ambaye alizaliwa Kijiji cha Kasumo, Wilaya ya Kasulu. Dk Mpango alizaliwa hapohapo Kasumo na ni kaka mdogo wa Askofu mstaafu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Tanganyika Magharibi – Kasulu mkoani Kigoma, Dk Gerard Mpango.

Dk Mpango ni mchumi mwenye shahada ya uzamivu ya uchumi. Hata hivyo, hadi sasa taarifa zake za elimu ya msingi, sekondari na shahada za awali za chuo kikuu hazijapatikana naye amekuwa vikaoni Dodoma muda mrefu na alishindwa kuzitoa kwa wakati.

Kuanzia miaka ya 1990 hadi 2000, alifanya kazi akiwa mhadhiri mwandamizi wa uchumi katika kitivo cha Biashara (sasa Shule ya Biashara) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Alikuwa akifundisha “Microeconomics”,

“Macroeconomics” (kwa mwaka wa pili) na “Public Finance” kwa mwaka wa tatu na kozi za uzamili.

Amewahi kuwa Mchumi Mwandamizi wa Benki ya Dunia, Mkuu wa Kamati ya kumshauri Rais Jakaya Kikwete wakati huo kuhusu masuala ya uchumi, Katibu binafsi wa Rais anayeshughulikia masuala ya uchumi, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, kabla ya kuhamishiwa Tume ya Mipango, Ofisi ya Rais. Nyadhifa hizi zote amezishika wakati wa utawala wa Kikwete.

Hayati Magufuli alipoingia madarakani alimteua kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na baada ya siku chache akateuliwa kuwa Waziri wa Fedha na Mipango.

Dk Mpango ni kiongozi mwenye msimamo thabiti. Baadhi ya watendaji ambao wamewahi kufanya kazi chini yake kwenye ofisi ya Rais wanamuelezea kama mtu anayetaka waliomzunguka wazungumze kwa takwimu na ushahidi hasa katika masuala ya uchumi. Msimamo huo pia aliuonyesha alipokuwa mtaalamu wa Benki ya Dunia. Hakuwa mwoga kuieleza ukweli Serikali pale ambako ilikuwa haifanyi vizuri.

Mathalan, wakati wasomi wengi wa uchumi wakiwa wanapiga kelele za kuisifia Serikali juu ya ukuaji wa uchumi miaka ya mwanzoni ya 2000, Dk Mpango alieleza wazi kuwa lengo hilo la kukuza uchumi kwa asilimia 5.9 haliwezi kufikiwa kwa sababu katika miaka minne iliyopita, Serikali ilishindwa kulifikia.

Alisema: “Angalia kwa miaka minne hadi mitano iliyopita ambayo tulikuwa na sera nzuri za kibajeti, hakuna mwaka ambao ukuaji huo ulifikiwa, hizo ni dalili tosha kwamba hali hiyohiyo ndiyo itajitokeza mwaka huu.”

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »