KIAMA CHA MAABARA BUBU CHATANGAZWA

KIAMA CHA MAABARA BUBU CHATANGAZWA

Na Mwandishi wetu Dar es Salaam Wamiliki wa Maabara bubu nchini ambazo hazijasajiliwa wamepewa kipindi cha mwezi mmoja kuanzia leo hadi Aprili 30 wawe wamesajili Maabara zao ili kuepuka kufungiwa. Agizo hilo limetolewa mapema leo na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Grace Magembe

Na Mwandishi wetu Dar es Salaam


Wamiliki wa Maabara bubu nchini ambazo hazijasajiliwa wamepewa kipindi cha mwezi mmoja kuanzia leo hadi Aprili 30 wawe wamesajili Maabara zao ili kuepuka kufungiwa.


Agizo hilo limetolewa mapema leo na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Grace Magembe wakati wa mkutano na Wamiliki wa Maabara binafsi za Mkoa wa Dar Es Salaam wenye kauli mbiu isemayo “Ushirikiano wa Wadau ni nguzo Muhimu katika utoaji wa Huduma Bora za Afya” uliofanyika katika ukumbi wa chuo cha Mwalimu Nyerere mkoani humo.


Dkt. Grace amesema kumekua na ongezeko kubwa la Maabara bubu nchini ambazo nyingine zinafunguliwa katika makazi ya watu na kusababisha kuhatarisha Maisha ya watu wanaokaa maeneo hayo hususani Watoto ambao wana tabia ya kuchezea vitu hatarishi.
“Nimetoa maelekezo kwa mratibu wa Maabara Mkoa wa Dar Es Salaam kuhakikisha maabara zote ambazo hazijasajiliwa zipewe nafasi ya kusajiliwa hadi kufikia tarehe 30 mwezi Aprili, kinyume na hapo zitafungiwa na wahusika kuchukuliwa hatua kwa kupelekwa kwenye vyombo vya sheria”. Amesema Dkt. Grace.
Dkt. Grace amesema huduma za Maabara ni huduma nyeti kwani zinahusika moja kwa moja na afya ya mwanadamu hivyo na endapo zitatoa majibu yasiyo sahihi zinaweza kuhatarisha Maisha ikiwa hatua stahiki hazitachukuliwa.


Aidha, Mkurugenzi huyo amesema kuna baadhi ya maabara ambazo hazina wataalamu wenye vigezo vinavyotakiwa au kuwa na upungufu kulingana na kazi zilizopo. Kutokana na hali hiyo, maabara hizo pia zimepewa mwezi mmoja hadi kufikia Aprili 30 wamiliki wa maabara hizo wawe wameshapata wataalamu wanaostahili kufanya kazi katika maabara hizo.

Pamoja na hayo, Dkt. Grace amewataka viongozi wa ngazi mbalimbali za mitaa, vijiji na vitongoji kutoa taarifa kwenye mamlaka husika endapo wataona kuna maabara zimeanzishwa katika maeneo yao ambazo hazijasajiliwa na kulipa ada.


Naye Msajili wa Maabara binafsi Ndg. Dominic John amesema lengo la Mkutano huo ni kuwaleta wataalamu na wamiliki wa maabara wa Mkoa wa Dar Es Salaam ili waweze kupata miongozo na namna ya kuendesha maabara zao kwa usahihi na kutoa huduma bora kwa wananchi.

Msajili wa Maabara binafsi Ndg. Dominic John

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »