Prof. Ndalichako agawa magari 38 yenye thamani ya Sh. Bilioni 6.

Prof. Ndalichako agawa magari 38 yenye thamani ya Sh. Bilioni 6.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako leo 31 Machi, 2021 amegawa magari 38 yenye thamani ya Sh. Bilioni 6 kwa Wathibiti Ubora wa Shule wa Kanda na Wilaya kwa lengo la kuimarisha shughuli za uthibiti ubora wa shule nchini. Akizungumza Jijini Dodoma katika hafla fupi ya ugawaji wa magari hayo, amesema suala

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako leo 31 Machi, 2021 amegawa magari 38 yenye thamani ya Sh. Bilioni 6 kwa Wathibiti Ubora wa Shule wa Kanda na Wilaya kwa lengo la kuimarisha shughuli za uthibiti ubora wa shule nchini.

Akizungumza Jijini Dodoma katika hafla fupi ya ugawaji wa magari hayo, amesema suala la usafiri ni la muhimu katika kuwawezesha Wathibiti ubora wa shule kuzifikia shule na vyuo vya ualimu kwa wakati ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.

“Wizara yangu ina jukumu la kusimamia mfumo wa uthibiti ubora wa shule na kufanya tathmini ya ujifunzaji na ufundishaji katika shule na vyuo vya ualimu na kutoa ushauri wa kitaalamu na kitaaluma ili kuinua ubora wa Elimu nchini, hivyo magari haya yatarahisisha na kuwezesha majukumu haya kufanyika kwa ufanisi na weledi,” amesema Waziri Ndalichako.

Wakati huohuo Profesa Ndalichako ametoa agizo kwa Wathibiti Ubora wa Shule wa Wilaya kuanza mara moja kukagua shule za sekondari badala ya kukagua shule za msingi pekee.

Amesema kuwa haileti maana yoyote kwa Mthibiti Ubora wa shule wa Wilaya kukagua shule za msingi pekee huku akiwa na sifa na mafunzo yanayomwezesha kukagua pia shule za sekondari.

Waziri Ndalichako amesisitiza kwamba agizo hilo linalenga kuimarisha matumizi mazuri ya fedha kwa kupunguza safari ambapo ukaguzi wa eneo moja umekuwa ukifanywa na Wathibiti ubora wawili tofauti wenye sifa na mafunzo yanayolingana.

Akiongea kwa niaba ya Wathibiti Ubora wa Shule, Victor Bwindiki ambaye ni Mkaguzi Mkuu wa Kanda ya Ziwa ameishukuru Serikali kwa jinsi inavyoendelea kuboresha mazingira ya kufanyia kazi na kuahidi kuendelea kutoa ushauri wa kitaalamu na kitaaluma kwa Walimu, Wakufunzi na Viongozi wa elimu ili kuinua ubora wa elimu nchini.

Magari yaliyotolewa yatapelekwa katika ofisi 10 za Kanda, 27 Ofisi za Halmashauri na moja litabaki Wizarani.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »