HOTUBA YA RAIS SAMIA LEO APRIL 06, 2021| SEKTA ALIZOCHAMBUA (+VIDEO)

HOTUBA YA RAIS SAMIA LEO APRIL 06, 2021| SEKTA ALIZOCHAMBUA (+VIDEO)

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo Aamewaapisha Viongozi walioteuliwa Aprili 04, 2021. Hafla ya uteuzi imefanyika Ikulu Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Viongozi wengine wa Kitaifa akiwemo Waziri Mkuu Walioapishwa ni Makatibu Wakuu na Naibu Wakatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali pamoja na Wakuu wa Taasisi kadhaa za Serikali ​HOTUBA YA RAIS SAMIA SULUHU

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo Aamewaapisha Viongozi walioteuliwa Aprili 04, 2021. Hafla ya uteuzi imefanyika Ikulu Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Viongozi wengine wa Kitaifa akiwemo Waziri Mkuu

Walioapishwa ni Makatibu Wakuu na Naibu Wakatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali pamoja na Wakuu wa Taasisi kadhaa za Serikali


HOTUBA YA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN
Rais Samia awapongeza viongozi wote walioteuliwa na kuapishwa pamoja na kutoa hotuba fupi.

“Nina salamu mpya nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mnatakiwa kuitikia kazi iendelee”

Rais Samia amesema “Watanzania tunakaribia Milioni 60 na zaidi ya Watanzania Elfu 5 walikuwa na sifa za kukaa mlipokaa leo lakini Mungu akaona nyinyi mpate nafasi, mlioapa leo nendeni mkafanye kazi”.

“TAMISEMI mbali na majukumu mengine mna jukumu la elimu na afya, Shule za Sekondari za Wanawake zina bajeti maalum naomba mkasimamie, tunatarajia kujenga Shule 26 mpaka 2025 naomba hili likatimie pamoja na kuendelea kujenga Hospitali za Wilaya”-Rais Samia.

“Natambua kuna Walimu wengi tu karibu Elfu 6 au zaidi ambao wamestaafu, wamefariki n.k na kunahitajika wakuziba nafasi hawa sio ajira mpya ni wa kuziba nafasi, Utumishi mko hapa na TAMISEMI mkalisimamie, Walimu Elfu 6 warudishwe haraka ili wakawatumikie Watanzania”

“Kuna ajira mpya za Madaktari upande wa afya, tumemaliza Hospitali na Vituo vingi, Bajeti ya mwaka huu ni kuweka vifaa na Watumishi kwahiyo Utumishi na TAMISEMI mkalisimamie hili la Watumishi na vitendea kazi kwenye huduma za afya”

“Tumezoea tunapokwenda kwenye ziara Mikoani na Wilayani, tunapokewa na mabango ya Wananchi wakilalalimikia kero mbalimbali na mabango yale sio mambo ya kushughulikiwa ngazi za juu, naomba tunapokuja Mimi, Makamu wa Rais, tukikuta bango iwe mambo ya Kitaifa”.

“Nataka niseme tukikuta bango moja aidha Mkurugenzi au Mkuu wa Wilaya umekwenda na hii haina maana mkazuie Watu kuandika kero zao, kero za Wananchi mkashughulikie na tukikuta malalamiko kwamba mnawafinya wasiseme hivyohivyo tutawashughulikia”.

“Naomba TAMISEMI mkakusanye mapato na matumizi yakafuate sheria na kanuni, nimemleta Mwana-Mama madhubuti (Ummy Mwalimu) nimempa Katibu Mkuu mzuri na Wasaidizi ni imani yangu kuwa kazi itafanywa”

“Najua TAMISEMI ni pamoja na Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi na hiyo kazi itafuata hivi karibuni (Uteuzi na Utenguzi), ili safu itimie na kazi iende ikafanywe….Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Kazi Iendelee)”.

AAIGIZA VYOMBO VYA HABARI VILIVOFUNGIWA KUFUNGULIWA
“Wizara ya Habari, nasikia kuna Vyombo vya Habari mmevifungia, sijui Viji- TV vya mikononi vile, vifungulieni lakini wafuate sheria na miongozo ya Serikali, tusiwape mdomo wa kusema tunabinya Uhuru wa Vyombo vya Habari, tusifungie tu kibabe”

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu ameitaka Wizara ya Habari kuwafungulia Vyombo vya Habari kama TV zilizofungiwa ila wafuate Sheria

Pia, ametaka Kanuni ziweke wazi makosa na adhabu zake ili kusiwe na ubabe kwa kuwa Serikali inaamini katika Uhuru wa Vyombo vya Habari

Aidha, ametaka Wasanii waangaliwe kwa umakini ili kukuza vipaji vinavyoibuka kila siku pamoja na kutunza tamaduni na silika ya Tanzania japo hatuna tamaduni moja

KUUNDWA KWA KAMATI YA COVID-19
“Tutaunda Kamati ya Wataalamu kuhusu Covid 19 watuambie kitaalamu hayo yanayopendekezwa na Ulimwengu kuja kwetu yapoje, hatuwezi kujitenga tu kama Kisiwa na hatuwezi kupokea yanayoletwa bila kuweka cha kwetu, bila kufanya utafiti wa kwetu”.

“Rais Kikwete alituambia akili za kuambiwa changanya na zako, tuweke na zetu tuwe na msimamo maalum unaoeleweka, sio tunasoma tu mambo ya Covid 19 Ulimwenguni, Tanzania deshi deshi deshi haieleweki, tueleweke kama tunakubali au tunakataa”.

“Suala la Covid 19 nafikikiria niunde Kamati ya Wataalamu waliangalie kwa upana wake kitaalamu halafu watushauri Serikali, halifai kulinyamazia aidha kulikataa au kulikubali bila kufanya Tafiti za kitaalamu”.

MABANDO YA SIMU
“Kuhusu suala la mabando kulizuka rabsharabsha juzi hapa, Wananchi wakapiga kelele mkalituliza, kalifanyieni kazi lisizuke namna ile mpo mnaangalia hawa Watu wanakuja tu na mambo yao mpaka Wananchi washtuke na nyie ndio mnashtuka, kakaeni nao”-

Mkeyenge NA TASAC
“Mkeyenge nimekuteua kuwa Mkuu wa Wakala wa Meli Tanzania (TASAC), ulikuwa TASAC unaijua vizuri karekebishe madudu yenu, moja kubwa ambalo limenichukiza sana kwa mwaka mmoja mmefanya vikao 23 vya Bodi na mmetumia karibu Milioni 600 na kitu kwa vikao vya Bodi tu”

“Mkeyenge ni Kijana nimekunyanyua wewe ni Kijana ukafanye kazi Wakala wa Meli (TASAC), hapa nitatumia ule msemo wa Aweso, wewe ni Kijana Mimi ni Mama ukinizingua tutazinguana, kafanye kazi pale na sio kwenda kunyanyua mabega kwa wenzio”

“Majina yalipotoka (ya uteuzi) Mitandaoo, siku ile nimelala saa kumi Alfajiri, Mitandaoni wanakuchambueni huyu hawezi, huyu hawezi, kwasababu ni majina mapya hatujayazoea, sasa nendeni mkaoneshe kuwa mnaweza, kafanyeni kazi”

“Wewe ni kijana, mimi ni mama, ukinizingua, tutazinguana.”

TRA NA KODI KWA WAFANYA BIASHARA
“TRA agizo langu kwenu ni kuacha matumizi ya ubabe na mabavu kwenye kukusanya kodi haisaidii, mtakwenda mtambinya Mtu, mtamkamua, mtamtisha na kupiga uhujumu uchumi anaogopa kwenda Jela atajikwangua atalipa lakini unaua biashara anafunga, kesho nani anakulipa kodi?

“Nendeni mkawe Wabunifu, sitegemei uzembe wa makusudi, nendeni mkafanye maamuzi, mnachelea sana kufanya maamuzi, kama mlichelea wakati ule sasa niko Mama, nimeshawaambia ukifanya ya hovyo tutazinguana, unataka kufanya umekwama njoo tuzungumze”.

Rais Samia Suluhu amewataka TRA wapunguze kutumia misuli katika ukusanyaji kodi na maduhuli kwa kuwa #Tanzania ndio wahitaji wa Wawekezaji japo Wawekezaji nao wanaihitaji Tanzania

Amesema kauli yake ya awali imefanya Wawekezaji wengi kuingia Nchini huku wengine wakitaka kuongea naye ili wahakikishiwe utaratibu wa kodi kwa mazingira ya Biashara.

Ametaja moja kati ya kesi ambayo aliyokutana nayo akiwa makamu wa Rais, ambapo baada ya Mwekezaji kutishiwa aliondoka na hakulipa kodi, kwa hiyo Tanzania ilikosa Mwekezaji na kodi waliyokuwa wanadai

Ametaka kuwe na mifumo mizuri ili kupunguza urasimu kwa wawekezaji wakitaka kuanzisha Biashara

AAGIZA WAWEKEZAJI KURUDI NCHINI
Nataka niwaambie wawekezaji wanalaumu, wanalalamika sana beaurecracy ya Serikali ya Tanzania. Kumekuwa na urasimu mkubwa, hakuna anayefanya maamuzi. Ukimwambia mtu Tanzania bana, they are unpredictable (hawatabiriki). Watu wanataka kuja Tanzania lakini kwa mambo yetu watu wanakimbia Tanzania.

Wanaosimamia kibali cha kazi, wamekuwa kama miungu watu, mtu akitaka kibali atazungushwa sana, nendeni mkatende haki, tunataka wawekezaji wafurahie uwekezaji.

Makampuni yanafungwa ndugu zangu sio uongo na wawekezaji wanaondoka, wakiondoka uchumi wetu unapungua na mzunguko wa fedha unapungua na hiki ndicho kilio cha Watanzania, mifuko mitupu

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »