WAZIRI JAFO: UPANDAJI MITI UWE ENDELEVU.

WAZIRI JAFO: UPANDAJI MITI UWE ENDELEVU.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo ameelekeza kuwa zoezi la upandaji miti liwe endelevu ili kusaidia kuhifadhi mazingira. Jafo ametoa agizo hilo leo Aprili 9, 2021 wakati akiongoza zoezi la upandaji miti lililofanyika katika eneo la Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) leo Aprili 9, 2021 lililoshirikisha wadau

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo ameelekeza kuwa zoezi la upandaji miti liwe endelevu ili kusaidia kuhifadhi mazingira.

Jafo ametoa agizo hilo leo Aprili 9, 2021 wakati akiongoza zoezi la upandaji miti lililofanyika katika eneo la Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) leo Aprili 9, 2021 lililoshirikisha wadau mbalimbali.

Akizungumza na wadau hao kutoka Kisima cha Mafanikio na Shirika la Kimataifa la Uhifadhi wa Mazingira (WWF) aliwataka kuendelea kuhamasisha wananchi kupanda miti.

“Naomba zoezi la upandaji miti liwe endelevu wananchi chukulie zoezi hili kama la kawaida wasisubiri Siku ya Mazingira ndo wapande miti, katika nyumba zetu angalau kila moja iwe na miti mitatu au minne na kwa pamoja tutaweza kuifanya Dodoma na Tanzania kwa ujumla kuwa ya kijani,” alisisitiza.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »