WAFANYAKAZI KIWANDA CHA MAGUNIA MOROGORO WASHANGAZWA KIWANDA KUFUNGWA BILA TAARIFA

WAFANYAKAZI KIWANDA CHA MAGUNIA MOROGORO WASHANGAZWA KIWANDA KUFUNGWA BILA TAARIFA

Na Frank Kaundula,  MOROGORO WAFANYAKAZI wa kiwanda cha magunia cha TPM 1998 Ltd mkoani Morogoro wamejikuta katika hali ya taharuki baada ya kiwanda hicho kusimamisha uzalishaji kwa madai ya kutokuwa na imani na kampuni ambayo waliipangisha kufanya uzalishaji kiwandani hapo kama inauwezo wa kuendelea na uzalishaji Wakizungumza nje ya geti la kiwanda hicho wafanyakazi hao wamesema kuwa

Na Frank Kaundula,  MOROGORO

WAFANYAKAZI wa kiwanda cha magunia cha TPM 1998 Ltd mkoani Morogoro wamejikuta katika hali ya taharuki baada ya kiwanda hicho kusimamisha uzalishaji kwa madai ya kutokuwa na imani na kampuni ambayo waliipangisha kufanya uzalishaji kiwandani hapo kama inauwezo wa kuendelea na uzalishaji

Wakizungumza nje ya geti la kiwanda hicho wafanyakazi hao wamesema kuwa wao walikuwa wanadi malipo ya muda wa ziada (overtime) ya mwezi wa tatu mwaka huu ambapo vilifanyika vikao kwaajili kutatua changamoto hiyo lakini wakashangazwa na hatua za ghafla zakufunga kiwanda bila taarifa.

Barnabas Paschal ni mwenyekiti wa chama cha wafanyakazi kiwandani hapo alisema awali walikaa kikao april 10 mwaka huu ambapo walikubalina malipo yatafanyika april 19 na wafanyakazi wakaendelea na shughuli ya uzalishaji kama kawaida

Alisema ilipofika siku ya jumatatu (juzi) wafanyakazi walifika katika vituo mbalimbali kusubiri usafiri wa kuwapeleka kiwandani bila mafanikio ndipo walipoamua kufika kiwandani kwa nauli zao na kushangazwa na kitendo cha kuzuiliwa kuingia kazini bili kupewa taarifa yaeyoye.

“baada ya kucheleweshewa overtime wafanyakazi waligoma ili wapewe majibu ya kinachoendela tuaahidiwa malipoyetu tutayapata tarehe 19 mwezi huu wan ne kwahiyo tukakubali kuendelea na kazi lakini leo ndio tumekuta geti limefungwa na hata usafiri wakutuleta hazini tatukupe” alisema Paschal

Naye Grace Lusubilo, meneja utawala na sheria RE OUT Consultance LTD  ambayo iliingia mkataba wa uzalishaji wa magunia kiwandani hapo alieleza kushangazwa na tukio hilo kwa kuwa hawakuwa na taarifa nalo ambapo hata viongozi wa kampuni hiyo walizuiliwa kuingia

Alisema kampuni yao iliingia mkataba kama waajili wa ambapo hulipwa na kampuni ya TPM 1998 kulingana na uzalishaji ambapo kwa mwezi machi walilipwa milioni 25 huku wakitakiwa kuwalipa wafanyakazi zaidi ya milioni 33

“ni kweli wafanyakazi wanadai malipo za ziada zaidi ya milioni 8 na wakurugenzi walikuwa katika mchkato wa kuipata hiyo fedha ndio mana tuliahidi hadi kufikia tarehe 19 april tuwe tumelia, kwasababu mwezi huu kampuni ilizalisha milioni 25 tu, sasa leo hatamimi sielewi maan nimezuiliwa kuingia kama wafanyakazi wengine” alisema Grace

 Akitoa ufafanuzi sababu za kufunga uzalishaji wa kiwanda hicho meneja wa utawala na sheria wa kiwanda hicho Nicodemas Mwaipaja alisema kuwa kampuni hiyo iliingia mkataba na ajira na kampuni ya RE OUT Consultance Ltd  kwaajili ya kufanya uzalishaji hapo.

Alisema kadri siku zinavyozidi kwenda uzalisjaji umekuwu ukishuka ambapo paoja na kuwalipa mshahara wao kampuni hiyo kushindawa kuwalipa wafanyakazi na kuingia deni la zaidi ya milioni 41.

“tumesitisha uzalishaji kwasababu hatuna inami tena nah ii kampuni ya  RE OUT Consultance Ltd  ambayo sisi tumeiajiri, mara kadhaa wamekuwa wakiingia migogoro na wafanyakazi kwasababu yakushindwa kuwalipa mishahara yao kutokana na kushuka  uzalishaji wao na wamekujakutkopa eni limefikia milioni 41” alisema Mwaipaja

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Morogoro Bakari Msulwa  akawataka viongozi wa kiwanda hicho kushughukia swala nilo nani ya muda mfupi na kutoa majibu ya uhakik juu ya hatima yawafanyakazi hao

Alisema kitendo cha kufunga kiwanda hicho bila kuwataarifu wafanyakazi ni kinyume na sheria na mikataba ya kazi walioingia bainayona kampuni walioiajili pamoja na wafanyakazi wengine

Aliwataka wafanyakazi wa  kiwanda hicho kuwa watulivu  wakati swala hilo linashughulikiwa ambapo majibu yatatolewa siku ya jumatano (leo).

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »