Wenyeviti wa mitaa sitini na nane katika manispaa ya Kigoma Ujiji mkoani Kigoma wameazimia kuishtaki halmashauri hiyo kwa kushindwa kualipa stahiki zao kwa zaidi ya miezi minane na wengine kudai madai ya zaidi ya miaka minne. Ucheleweshwaji wa malipo ya madai hayo umefanya wenyekiti hao kukutana kujadili mustakabali juu ya malipo hayo ikiwemo kwenda mahakamani
Wenyeviti wa mitaa sitini na nane katika manispaa ya Kigoma Ujiji mkoani Kigoma wameazimia kuishtaki halmashauri hiyo kwa kushindwa kualipa stahiki zao kwa zaidi ya miezi minane na wengine kudai madai ya zaidi ya miaka minne.
Ucheleweshwaji wa malipo ya madai hayo umefanya wenyekiti hao kukutana kujadili mustakabali juu ya malipo hayo ikiwemo kwenda mahakamani kwani wenyeviti waliomaliza muda wao wanadai laki tisa na elfu arobaini kila mmoja huku walioko madarakani kwa sasa wakidai laki moja na elfu stini, na kwamba wamehangaika kwa kipindi kirefu sana kudai posho hizo bila mafanikio licha ya kiwango hicho kuidhinishwa kisheria kama stahiki yao kwa kila mwezi.
Akitoa majibu juu ya madai hayo,mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya manispaa ya Kigoma Ujiji MWAILWA PANGANI amekiri manispaa hiyo kudaiwa na kueleza tayari wameanza taratibu za tathmini.
Leave a Comment
Your email address will not be published. Required fields are marked with *