MIQUISSONE ATWAA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA MWEZI MACHI

MIQUISSONE ATWAA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA MWEZI MACHI

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KIUNGO wa pembeni wa Simba SC ya Dar es Salaam, Luis Miquissone amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Machi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania (VPL) msimu wa 2020/21, huku Mohammed Badru wa Gwambina FCakichaguliwa Kocha Bora wa mwezi huo. Miquissone na Badru walitwaa tuzo hizo, baada ya kuwashinda wenzao

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


KIUNGO wa pembeni wa Simba SC ya Dar es Salaam, Luis Miquissone amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Machi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania (VPL) msimu wa 2020/21, huku Mohammed Badru wa Gwambina FC
akichaguliwa Kocha Bora wa mwezi huo.


Miquissone na Badru walitwaa tuzo hizo, baada ya kuwashinda wenzao walioingia nao fainali kwa mwezi Machi katika uchambuzi uliofanywa wiki hii na Kamati ya Tuzo za VPL, kutokana na mapendekezo ya makocha waliopo vituo mbalimbali
ambavyo ligi hiyo inachezwa.


Kwa Machi, Miquissone alikuwa na mchango mkubwa kwa timu yake na kuonesha kiwango cha kuvutia, ambapo Simba ilishinda mchezo mmoja na kutoka sare mmoja, huku mchezaji huyo akifunga mabao mawili na kuchangia bao
moja.

Wachezaji wengine walioingia fainali ni Idd Selemani wa Azam FC na Paul Nonga wa Gwambina FC.
Kwa upande wa Badru alitwaa tuzo hiyo baada ya kuiongoza Gwambina kushinda michezo miwili na kutoka sare mmoja na kupanda kutoka nafasi ya 15 hadi ya 11 katika msimamo wa ligi hiyo. Gwambina ilishinda michezo miwili ugenini ikiifunga Ihefu SC 1-2, pia ikaifunga Mtibwa Sugar FC 0-2 na kutoka 0-0 nyumbani dhidi ya Polisi Tanzania FC.


Wachezaji wengine ambao tayari wameshatwaa tuzo hiyo ya mwezi kwa msimu huu na miezi yao katika mabano ni Prince Dube wa Azam (Septemba), Mukoko Tonombe wa Yanga (Oktoba), John Bocco wa Simba (Novemba), Saido
Ntibazonkiza wa Yanga (Disemba), Deogratius Mafie wa Biashara (Januari) na Anuary Jabir wa Dodoma Jiji (Februari).


Makocha waliotwaa tuzo hiyo ni Aristica Cioaba aliyekuwa Azam (Septemba), Cedric Kaze aliyekuwa Yanga (Oktoba), Charles Mkwassa wa Ruvu Shooting (Novemba), Cedrick Kaze aliyekuwa Yanga (Desemba), Francis Baraza aliyekuwa
Biashara United (Januari) na Zuberi Katwila wa Ihefu (Februari).


Pia Kamati ya Tuzo imemchagua Meneja wa Uwanja wa Sokoine, Mbeya Modestus Mwaluka, kuwa mshindi wa Tuzo ya Meneja Bora wa Uwanja kwa mwezi Machi. Hivi karibuni TFF ilianzisha Tuzo ya Meneja Bora wa Uwanja ambayo itakuwa ikitolewa kila mwezi ikiwa ni sehemu ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL).


Ushindi wa Meneja huyo umefuatia kufanya kwake vizuri katika Menejimenti ya matukio ya michezo iliyofanyika kwenye uwanja huo kwa Machi pamoja na masuala yanayohusu miundombinu uwanjani.


Lengo kuu la tuzo hiyo ni kuhamasisha Mameneja wa viwanja kutilia mkazo masuala ya menejimenti ya matukio, kutunza na kusimamia miundombinu ya viwanja na taratibu nyingine zinazohusu mpira wa miguu katika viwanja vyao.


TFF imekuwa na utaratibu wa kutoa Tuzo ya Mchezaji Bora na Kocha Bora wa VPL kila mwezi, ambapo pia mwisho wa msimu kunakuwa na tuzo za wachezaji mbalimbali waliofanya vizuri kwa msimu mzima, ikiwemo Tuzo ya Mchezaji
Bora wa Tanzania. Pia kwa mara ya kwanza kutakuwa na Tuzo ya Meneja Borawa Uwanja kwa msimu.


Idara ya Habari na Mawasiliano
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB)
Aprili 19, 2021

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »