RC CHALAMILA AWAKEMEA WANAOMUONGEA VIBAYA HAYATI RAIS MAGUFULI

RC CHALAMILA  AWAKEMEA WANAOMUONGEA VIBAYA HAYATI RAIS MAGUFULI

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albart Chalamila amefikia hatua ya kusema hayo baada ya kuona watu wanasaau kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kujiletea Maendeleo katika Kaya Zao na Serikali na badala yake wanakaa na kumjadili aliyekuwa Rais wa Jamuhuri ya Muhungano wa Tanzania, Hayati Daktari John Pombe Magufuli na kumsema alikuwa mbabe. Chalamila ameyasema

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albart Chalamila amefikia hatua ya kusema hayo baada ya kuona watu wanasaau kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kujiletea Maendeleo katika Kaya Zao na Serikali na badala yake wanakaa na kumjadili aliyekuwa Rais wa Jamuhuri ya Muhungano wa Tanzania, Hayati Daktari John Pombe Magufuli na kumsema alikuwa mbabe.

Chalamila ameyasema hayo akiwa Wilayani Chunya Mkoani Mbeya wakati akiongea na wachimbaji wadogo wa Madini na kuwataka kuendelea kuchapa kazi, Kama ambavyo Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassani anavyosema kazi ziendelee.

“wengine nimesikia kwenye mijadala Rais Magufuli alikuwa dikteta ukimwona mtu anatokea sasa ivi anaanza kuongea wakati aliekuwa Rais amefariki ujue huo ni mjadala hewa,sasa ndugu zangu msijiingize kwenye Mijadala hiyo, mjadala sahihi utakao tutoa kimaisha ni kazi sio mijadala hewa kwasababu kama kuongea jambo lenye maana basi ilifaa mfikishie ujumbe wakati akiwa hai mkianaza kueleza mambo ambayo yeye amefariki mnatuchosha akili nazo stack

Tunataka mfanye kazi, ndio maana na sisi tumekuja hapa kuwaamasisha kuwa mwendelee na kazi mjadala wa kweli ni kazi iendeleemjadala wa kweli nikuuliza umeme uko wapi,mjadala wa kweli nikuuliza mbona barabara haijatengenezwa, mjadala wa kweli nikusema mbona mawasiliano hamna, mjadala wa kweli nikusema hapa kuna watu wanatudai kodi wanatunyanganya kwa nguvu,mjadala wa kweli ni tupate vituo vya afya vizuri, mjadala wa kweli tupate shule nzuri,mjadala wa kweli tuwe na maisha bora mijadala hewa tuipotezee haitatufikisha tunakokwenda.”

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »