IDRISS DEBY: RAIS ALIYEINGIA MADARAKANI KWA MTUTU NA KUNG’OLEWA KWA MTUTU

IDRISS DEBY: RAIS ALIYEINGIA MADARAKANI KWA MTUTU NA KUNG’OLEWA KWA MTUTU

Idriss Déby, rais wa Chad kwa miaka 30, alikuwa ni mpambanaji. Aliingia madarakani kwa mtutu wa bunduki na ametoka kwa mtutu wa bunduki. Rais huyo mwenye miaka 68, ambaye alikuwa amechaguliwa kuliongoza taifa lake kwa muhula wa sita ameuawa vitani na waasi, na kuandikisha ukomo wa mtawala ambaye alisifika kwa uwezo wake vitani. Alipokea mafunzo

Idriss Déby, rais wa Chad kwa miaka 30, alikuwa ni mpambanaji.

Aliingia madarakani kwa mtutu wa bunduki na ametoka kwa mtutu wa bunduki.

Rais huyo mwenye miaka 68, ambaye alikuwa amechaguliwa kuliongoza taifa lake kwa muhula wa sita ameuawa vitani na waasi, na kuandikisha ukomo wa mtawala ambaye alisifika kwa uwezo wake vitani.

Alipokea mafunzo ya kijeshi nchini Ufaransa na kufuzu kama rubani wa ndege za kivita. Alirudi kutoka Ufaransa mnamo Februari 1979 na kukuta Chad imekuwa uwanja wa vita kwa vikundi vingi vyenye silaha. Déby alijiunga wale wa Hissène Habré, mmoja wa wakuu wa wapiganaji nchini Chad. Mwaka mmoja baada ya Habré kuwa rais mnamo 1982, Déby alifanywa kamanda mkuu wa jeshi.

Alijijengea sifa mnamo 1984 kwa kuharibu vikosi vinavyoiunga mkono Libya mashariki mwa Chad. Mnamo 1985, Habré alimtuma Paris kufanya mafunzo huko École de Guerre; aliporudi mnamo 1986, alifanywa mshauri mkuu wa jeshi kwa ofisi ya rais. Mnamo 1987, alikabiliana na vikosi vya Libya uwanjani, akisaidiwa na Ufaransa katika kile kinachoitwa “Vita vya Toyota”, akitumia mbinu ambazo zilisababisha hasara kubwa kwa vikosi vya maadui.

Uhasama hata hivyo uliibuka mnamo Aprili 1989 kati ya Habré na Déby juu ya nguvu iliyoongezeka ya kikosi cha Walinzi wa Rais. Kulingana na Human Rights Watch, Habré alipatikana na hatia ya “mauaji ya kisiasa yaliyotokana na mateso, na maelfu ya watu kukamatwa kiholela”, pamoja na mauaji ya kikabila wakati ilipogundulika kuwa viongozi wa makundi mbali mbali wanaweza kuwa tishio kwa utawala wake, pamoja na wengi wa kabila la Zaghawa la Déby ambao waliunga mkono serikali.

Habré alimtuhumu Déby, waziri wa mambo ya ndani Mahamat Itno, na kamanda mkuu wa jeshi la Chad Hassan Djamous kwa kuandaa mapinduzi. Déby alikimbilia kwanza Darfur, kisha Libya, ambapo alikaribishwa na Gaddafi huko Tripoli. Itno na Djamous walikamatwa na kuuawa.

Kiongozi wa Libya wakati huo, Kanali Muammar Gaddafi – alikuwa adui mkubwa wa Habré – na alimsaidia Déby kuanzisha uasi kwa malipo ya taarifa juu ya operesheni za CIA nchini Chad.

Déby na wafuasi wake waliuteka mji mkuu wa N’Djamena mwezi Disemba 1990 – hata hivyo alikabiliana na mlima wa changamoto pamoja majaribio lukuki ya mapinduzi ya kijeshi katika miaka 30 iliyopita.

Mwaka 2016, waasi walikuwa wakivurumisha mabomu nje ya ikulu yake na mwaka 2008-2009 wakati waasi wakikaribia mji mkuu alichimba mahandaki kuuzingira mji huo na kukata miti yote mikubwa ili kuwazuia kupenya.

Aliogopwa na alitisha
Waangalizi wa mambo wanasema si jambo la kushangaza kusikia Déby amefariki mstari wa mbele kwa kuwa alikuwa akifanya hivyo kukabiliana na uasi kila pale alipoona makamanda wake hawakuwa wakiongoza vyema mapambano.

Mwaka 2008 alilazimika kuchimba mahandaki ili kuwazuia waasi kuuteka mji mkuu wa N’Djamena


Akiwa kama kamanda wa jeshi na rais aliogopwa – watu wanasema alikuwa na hali ambayo hakuna mtu ambaye angeweza kumchezea.

Na hakuogopa kutumia mabavu kushughulikia aina yoyote ya hatari kwake.

Vita vya kijihadi

Déby alithibitisha hilo kwa kuwa mtu muhimu katika vita dhidi ya wanamgambo wa Kiislamu katika jimbo la Sahel – eneo lenye ardhi kame lililo kusini mwa jagwa la sahara na linaloshirikisha mataifa ya Mali, Chad, Niger, Burkina Fasso na Mauritania.

Wanajeshi wa Déby wakielekea uwanja wa vita jangwani


Wakati wanajeshi wa Nigeria waliposhindwa kulikabili kundi la Boko Haram kaskazini mashariki mwa Nigeria 2015 na huku hali ya utovu wa usalama ikisambaa katika mataifa mengine yanayopakana na Ziwa Chad ,Deby alituma wanajeshi wake nchini Nigeria.

Wanajeshi wake pia wamekuwa kiungo muhimu katika kikosi cha G5, kilichobuniwa baada ya Ufaransa kuingilia kati nchini Mali mwaka 2013 ili kuzuia kunyakuliwa na makundi ya wanajihad.


Deby pia alionesha jinsi vita vinavyopigwana katika eneo hilo wakati alipoongoza vikosi vya Chad dhidi ya jeshi lenye uwezo mkubwa la Libya 1987.

Katika kile kilichokuwa vita vya Toyota, alitumia magari yenye kasi kuu aina ya Pick up yaliobeba makombora na bunduki kali ili kuwashinda wanajeshi hao wa Libya, mbinu inayotumika hadi sasa katika eneo hilo.

Mapato ya mafuta kuchezewa


Déby alizaliwa kaskazini mwa Chad mwaka 1952, miaka minane kabla ya nchi hiyo kupata uhuru kutoka Ufaransa. Baba yake akiwa ni mfugaji kutoka ukoo wa Zaghawan.

Baadhi ya wakosoaji wake wanasema makosa yake makubwa yalikuwa ni kupendelea ukoo wake badala ya nchi yake.

Lakini namna ambavyo ametumia mapato ya mafuta ndiyo jambo ambalo yawezekana amelikosea zaidi.

Chad ilianza kuzalisha mafuta mwaka 2003 baada ya kumalizika ujenzi wa bomba la thamani ya dola bilioni 4 likiunganisha visima vya nchi hiyo na bahari ya Atlantiki.

Wadadisi wanasema Déby alitumia vibaya mabilioni kwa mabilion ya mapato kutoka kwenye mafuta na hakutekeleza miradi yoyote mikubwa ya maendeleo.

Umaskini nchini Chad ni mkubwa na kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) kuna madaktari chini ya wanne kwa kila watu 100,000 nchini humo.

Kutokana na namna ambavyo aliitawala nchi hiyo kwa miongo mitatu iliyopita, kifo cha Déby kinaliacha taifa hilo katika njia panda na hali inaweza kuwa mbaya zaidi ya ilivyowahi kuwa kabla.

#BBC

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »