“Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” SHUKRANI“Mheshimiwa Spika mbali ya kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema na rehema zake, imekuwa ni miaka takribani sita imepita tangu niondoke kwenye jengo hili adhimu la bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hivyo leo ninayo furaha ya kurudi tena na kupata fursa ya kulihutubia bunge ambalo
“Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,”

SHUKRANI
“Mheshimiwa Spika mbali ya kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema na rehema zake, imekuwa ni miaka takribani sita imepita tangu niondoke kwenye jengo hili adhimu la bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hivyo leo ninayo furaha ya kurudi tena na kupata fursa ya kulihutubia bunge ambalo limenilea limenijenga, limeninoa na ni bunge hili lililofanya uwezo wangu uonekane na wote mpaka kushika nafasi hii niliyonayo.”
“Nawashukuru sana Marais Wastaafu, uwezo wangu wa Uongozi uliibuliwa na Rais Karume aliyenipa nafasi ya Uwaziri, malezi haya yaliendelezwa na Dr.Kikwete aliyenipa Uwaziri na baadaye Makamu Mwenyekiti wa Bunge la Katiba, nimshukuru pia Hayati Magufuli kwa kuniamini.”

“Kuniamini kwa Hayati Magufuli kuwa Mgombea Mwenza wake kumeniwezesha leo hii kuwa Mwanamke wa Kwanza Tanzania kushika nafasi ya Umakamu wa Rais na hatimaye sasa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania”
“Nimekuja kulihutubia Bunge baada ya Nchi yetu kupita kwenye kipindi kigumu, kama inavyokumbukwa March 17 Taifa letu lilipata msiba mkubwa wa kuondokewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Magufuli,hivyo tusimame kumuombea Mpendwa wetu”
“Mapenzi ya Watanzania kwa Hayati Magufuli yalidhihirika katika kipindi cha maombolezo ambapo wengi walijitokeza kumuaga, namshukuru Mungu kwa kutupitisha salama kwenye kipindi cha mabadiliko ya Uongozi, dhamana hii ni kubwa na yenye mitihani mingi”

Ni ukweli kwamba Hayati Dkt. Magufuli alikuwa kiongozi jasiri na shupavu mwenye maono ambaye aliipenda Nchi yetu. Natumia fursa hii kutoa pole tena kwa Mama wa Rais, Mama mjane Janeth, Watoto na familia. Pia, natoa pole kwa Bunge hili na kwa Watanzania wote.
Nakishukuru Chama changu cha CCM kwa kunijengea uwezo mkubwa na wakati wote kimeniamini kwani wasingeniamini nisingekuwa mbele yenu. Nawashukuru Viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali na nawashukuru kwa dhati Marais wastaafu wote na Viongozi wakuu wa Kitaifa.
Niseme wazi, kwa uwezo wangu wa uongozi uliibuliwa na Amani Karume aliyenipa nafasi ya Uwaziri katika kipindi changu nikiwa Mjumbe wa Baraza la Mawaziri Zanzibar Malezi yaliendelezwa na Jakaya Kikwete aliyenipa Uwaziri na baadaye kuwa Makamu M/Kiti wa Bunge la Katiba.
Nalishukuru Bunge kwa ushirikiano mkubwa ambao limenipa tangu nilipochukua dhamana ya kuongoza Nchi yetu. Nalishukuru kwa kupitisha adhimio la kunipongeza na kuahidi ushirikiano. Pia, kupitisha pendekezo langu la kumpitisha Dkt. Mpango kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Rais samia pia Kamshukuru Rais wa Zanzibar, Vyombo vya Ulinzi na usalama pamoja na Wageni wote waalikwa, Vyombo vya habari na Watanzania wote kwa kumuamini na kumuunga mkono. Aidha, baada ya shukrani Rais Samia amesema yafuatayo:
Dira na mwelekeo wa Serikali ya Awamu ya 6 utakuwa ni kudumisha yale ya Serikali zilizopita. Tutaendeleza mema na kuibua yaliyo mapya. Jambo la kwanza ambalo tutalipa kipaumbele ni kuendelea kulinda na kudumisha Tunu za Taifa letu. Amani, Umoja na Mshikamano.
Amani na Umoja ni Msingi Mkuu ndani ya Taifa lolote. Hivyo nawasihi Watanzania kila mmoja tushirikiane kuzilinda na kuzitunza Tunu hizi. Tanzania ni yetu sote. Kila mmoja wetu anao wajibu wa kuhakikisha anazilinda na kuzitunza Tunu hizi
“Niliwahi kusema na leo narudia tena kwamba Mimi na Hayati Magufuli ni kitu kimoja, kwahiyo mengi ambayo nimepanga kuyatekeleza ni yale ambayo yalielezwa na Hayati Magufuli wakati akilizindua Bunge hili”.
Pia, tunakusudia kuelekeza nguvu kubwa katika ukuzaji wa Uchumi. Taifa letu limepata mafanikio makubwa kiuchumi hususan miaka 5 iliyopita. Takwimu zinaonyesha kwa Tanzania Uchumi wetu tumeusimamia kwa wastani wa 6.9% na kudhibiti Mfumuko wa Bei kwa 4.4%. Na kupuza umasikini kwa kiwango cha asilimia 26.6%.
Muhimu zaidi Mwaka jana mwezi julai Taifa letu lilifanikiwa kuingia Uchumi wa Kati ambapo Pato la Wastani wa kila Mtanzania limeongezeka hadi kufikia dola 1080 zaidi ya kigezo cha dola 1036 cha kuingia kwenye kundi hilo. Hayo bila shaka ni mafanikio makubwa. Jitihada zaidi zinahitajika ili kuongeza kasi ya ukuaji Uchumi na kupambana na umasikini nchini. Hii ni kwa sababu licha ya mafanikio tuliyoyapata kasi ya ukuaji wa uchumi bado ni ndogo.
UKUAJI WA UCHUMI NA UWEKEZAJI
Wataalamu wa Uchumi wanatueleza kwamba ili kuweza kupambana na umasikini uchumi wetu unatakiwa ukue kwa angalau asilimia 8 kwa mwaka. lakini kutokana na Dunia kukumbwa na janga la Corona, kiuhalisia takwimu zinaonesha kwa chumi nyingi duniani zimeshuka. Tanzania nayo imeathirika kutoka wastani wa ukuaji wa uchumi wa 6.9% hadi 4.7%.
Hii inamaanisha kwamba katika miaka mitano ijayo tunahitajika uwekezaji mkubwa sana katika sekta za uzalishaji na zinazotoa ajira kwa wingi. Hatua mahsusi tutakazozichukua katika kukuza uwekezaji ni pamoja na kufanya marekebisho kadhaa katika sera, sheria na kanuni zetu na kuondoa vifungu vitakavyosababisha vikwazo katika kukuza uwekezaji.
“Tutarudisha imani ya Wawekezaji na kutoa vivutio kwa Wawekezaji, tunalalamikiwa sana, kumekuwa na mchakato mrefu Watu wanapotaka kuwekeza Tanzania, Serikali ya Awamu ya Sita tunakwenda kukomesha hili na Uwekezaji utakwenda kwa haraka”.
Kuna ucheleweshwaji wa vibali kwa Wafanyabiashara wa Kigeni, kuna usemi unasema ukiona Mtu Mzima analia ujue kuna jambo, tutashughulikia hili huku tukilinda maslahi ya Taifa. Tutachukua hatua madhubuti kuboresha mazingira ya biashara, kutoa vivutio kwa Wawekezaji
ULIPAJI WA KODI
“Tutaweka mifumo rafiki ulipaji kodi , ningependa kuona Wafanyabiashara wanalipa kodi bila matumizi ya nguvu wakitambua kwamba kodi ni maendeleo yao, kumekuwa na matumizi ya nguvu wakati wa ukusanyaji kodi hili tutalikomesha”.
”Watanzania wachache ndio wanaolipa kodi, hivyo kuna haja ya kutanua wigo wa walipa kodi, ningependa kuona wafanyabiashara, wawekezaji na wananchi wanalipa kodi bila shuruti na bila matumizi ya nguvu wakitambua kwamba kodi ni maendeleo yao”
“Mashirika mengi ya Umma yanaendeshwa kwa kusuasua, ikifika wakati wa kutoa gawio Serikalini Viongozi wa Mashirika hayo wanahangaika kutafuta gawio wakihofia nafasi zao, tutaboresha Mashirika ya Umma ili yawe na tija na kuzalisha faida”.
KUHUSU KILIMO NA UFUGAJI
Tunakusudia kuongeza maeneo ya Ufugaji, lengo likiwa ni kuepusha Wafugaji kuhama hali inayopelekea uharibifu wa mazingira na migogoro ya ardhi Tunatarajia kununua meli 8 za uvuvi ili zishiriki ktk Uvuvi wa Bahari Kuu, nne zitafanya kazi Zanzibar na nne Tanzania Bara.
Tunalenga kuachana na uchungaji wa kuhama hama kwani hauna tija. Katika ufugaji huu Ng’ombe hanenepi wala Mchungaji hanenepi – Katika miaka hii mitano tutawekeza katika kutoa Elimu ya Ufugaji wa kisasa na kuongeza uzalishaji wa vyakula vya mifugo viwandani.
Sekta ya Kilimo kwa sasa inachangia asilimia 100 ya chakula kinacholiwa nchini, asilimia 60 ya malighafi za Viwandani, asilimia 27 ya Pato la Taifa na asimilia 25 ya Fedha za Kigeni. Hata hivyo bado Sekta hii inakabiliwa na changamoto nyingi.
”Katika miaka mitano tunayokwenda nayo tutaendelea kuongeza nguvu kuhakikisha kilimo kinakuwa na tija, ikiwemo kuwa na mbegu bora, kuboresha afya ya udongo, pamoja na kuziwezesha taasisi za kilimo kwa kuzipa fedha ili ziweze kuzalisha kwa tija”.
Ili kukuza zaidi Sekta ya Kilimo hatuna budi kufungamanisha Sekta ya Kilimo na Sekta ya Viwanda. Viwanda vinawahakikishia wakulima soko la mazao yao – Tutaendeleza jitihada za kuhamasisha ujenzi wa Viwanda hususani vinavyotumia malighafi za hapa Nchini.
Tunafahamu Nchi yetu imebarikiwa Vivutio vya Utalii, ambapo Sekta hii ya Utalii imeajiri Watanzania milioni 4 – Mafanikio mengi yamepatikana ikiwemo kuongezeka kwa mapato kutoka dola za Kimarekani bilioni 1.9 mwaka 2015 hadi dola bilioni 2.6 mwaka 2019
USAFIRI WA ANGA NA ATCL
Katika Usafiri wa Anga, tutaendelea kupanua na kukarabati Viwanja vya Ndege Mikoani ikiwemo kujenga Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa hapa Makao Makuu, Dodoma. Pia, tutaendelea kulilea Shirika letu la Ndege ATCL kimkakati ili lijiendeshe kibiashara.
”Kuilea ATCL kimkakati ni pamoja na kuangalia uwezekano wa kutoa unafuu wa madeni na baadhi ya kodi na tozo kama inavyofanyika kwenye nchi nyingine ili liweze kukua na kuweka mahesabu yake sawa, kwasasa halina thamani kwasababu ya kurithi madeni makubwa ya nyuma”.
”Kama serikali tunakwenda kulitua mzigo mkubwa shirika letu la ATCL ili liweze kukua, tutajitahidi kuepuka mambo yote yasiyo na tija kwa shirika letu, hatutakubali kuona shirika linaendelea kupata hasara baada ya uwekezaji mkubwa tuliofanya” .
Tunakwenda kufanya utafiti wa kina ili kuhakikisha tutakaowaamini kuliendesha Shirika letu la Ndege wana weledi na uwezo wa kuliendesha shirika hili kibiashara. Pia, tutakamilisha Ujenzi wa Mradi wa Kufua Umeme wa Mwl. Nyerere ili nchi kuwa na nishati ya kutosha.
MAWASILIANO NA TEHAMA
Uchumi na shughuli nyingi duniani kwa sasa zinafanyika kupitia TEHAMA, nasi Tanzania tunapaswa kufikia huko – Katika kipindi cha miaka mitano tumepanga kuboresha na kufikisha huduma ya Mkongo wa Taifa katika Ngazi za Wilaya.
Tunapanga kuongeza wigo wa matumizi ya Mawasiliano ya Kasi yaani ‘Broadband’ kutoka asilimia 45 ya sasa hadi 80 mwaka 2025. Aidha, tutaongeza watumiaji wa intaneti kutoka asilimia 43 ya sasa hadi 80% mwaka 2025. Pia, tutaboresha Mawasiliano ya Simu nchi nzima.
KUHUSU AFYA NA CORONA
Serikali itaboresha Huduma za Afya na kupunguza vifo vya Mama na Mtoto kwani hatupendi kuona watu wakifariki kwa sababu zinazoweza kuepukika. Ninasikitishwa sana Watanzania milioni 8.2 tu (sawa na 14% ya Watanzania wote) ndio wenye Bima ya Afya.
Serikali itaboresha Huduma za Afya na kupunguza vifo vya Mama na Mtoto kwani hatupendi kuona watu wakifariki kwa sababu zinazoweza kuepukika – Ninasikitishwa sana Watanzania milioni 8.2 tu (sawa na 14% ya Watanzania wote) ndio wenye Bima ya Afya.
Hadi sasa hakujapatikana kinga ya Ugonjwa wa Covid 19, tumeunda Tume maalumu ambayo itashirikiana na Taasisi za Afya kuliangalia suala hili kiundani na kutoa mapendekezo ya namna ya kupambana na janga hili.
Wakati tukisubiri majibu ya Kamati ya Wataalamu wa Corona iliyoundwa, nichukue fursa hii kuwataka Watanzania kuchukua tahadhari kwani ulinzi wa afya yako, unaanza na wewe mwenyewe, usisubiri tamko la Serikali.
UHURU NA DEMOKRASIA
Katika kulinda Uhuru wa Kidemokrasia nakusudia kukutana na Viongozi wa Siasa – Uhuru na Demokrasia ni Msingi wa Amani katika nchi na hakuna Uhuru wa Kidemokrasia usiosimamiwa na Sheria. Niwaombe Watanzania kufanya mambo yetu kwa kufuata Sheria.
MAJI
Ninakwenda kufanya marekebisho makubwa kwa Wahandisi wa Maji Mikoani. Fedha nyingi zimekuwa zikitoka lakini kumekuwa na kusuasua. Waziri wa Maji ile kauli yako ya ‘ukinizingua tunazinguana’ inarudi kwako. Tunakwenda kutunisha Mfuko wa Maji na kuondosha utendaji mbovu.
Tatizo kwenye maji ni kusuasua. Walioshindwa kutuletea maji na kutumia fedha nyingi wakae upande tuingize damu mpya. Lengo ni kufikisha maji kwa asilimia 95 Mijini na asilimia 85 Vijijini ifikapo mwaka 2025. Tupeleke maji kwa Wananchi kwa haraka.
Lingine tutakalolifanya ni utunzaji wa Vyanzo vya Maji pamoja na mazingira. Kwa maeneo ambayo hayana kabisa vyanzo vya maji tunakwenda kuchimba visima vya kuvuna maji ya mvua – Pia, tutaziimarisha Kamati za Maji Mitaani na Vijijini ili ziweze kusimamia miradi yao.
UCHONGANISHI KUHUSU KIFO CHA HAYATI MAGUFULI
Kila Mtu Duniani atapata umauti na kila mauti ina sababu. Nimeona kwenye Mitandao taarifa za uchonganishi – Taarifa tuliyopewa na Madaktari ya kifo cha Magufuli ni Tatizo la Moyo. Nimekua naona mitandaoni wanasema fulani na fulani wamempa sumu, waache hili.
Wanaosema mitandaoni kuwa Hayati Magufuli alipewa sumu, mara fulani na fulani walitega kitu, kama wana taarifa za maana waje tuwasikilize, lasivyo waache kuleta uchonganishi. Kama wanafanya hivyo kwasababu hatutowapata warudi kwa Mungu wajiulize je, wanafanya sawa?
Wanaoleta uchonganishi kwenye Mitandao nadhani wanafanya hivyo kwasababu wanajua hatutoweza kuwapata – Wanatumia mifumo hiyo huko kwingine ambayo bado hatujawa na uwezo wa kuwatafuta, lakini niwaambie tutawatafuta
RAIS MWANAMKE
Hii ni mara ya 1 kwa Taifa letu kupata Rais Mwanamke na hivyo najua kuna watu wenye wasiwasi kwamba kutokana na jinsia yangu sitaweza kuyatimiza niliyoyasema hapa. Naomba nitumie Bunge hili kusema kwamba Mwenyezi Mungu hakuumba ubongo dhaifu kwa mwanamke.
KUWAKOSOA VIONGOZI
Haya niliyoyasema hapa sio kwamba nakwenda kuyafanya peke yangu. Nitakaa na kushirikiana na wenzangu. Tukosoeni pale inapobidi na naomba mtukosoe vikali sana. Mawaziri wangu wakileta vitu visivyoeleweka wakosoeni vikali sana, lakini wakosolewe kwa lugha ya kibunge.
Kuna baadhi ya watu wameenza kulegalega na wizi umeanza kushamiri kwenye baadhi ya maeneo. Nataka niwaambie kwamba mwendo ni ule ule.
Niwaonye wale wote wanaosimamia mali za Umma, ukwepaji kodi, ubadhirifu, kukemea uzembe na uvivu kuwa yameondoka kutokana na kuondoka kwa Hayati Magufuli – Amekwenda peke yake, lakini maoni na mikakati tunaifanyia kazi
Leave a Comment
Your email address will not be published. Required fields are marked with *