MAKAMU WA RAIS ZANZIBAR ATOA ZAWADI KWA MSHINDI WA KUHIFADHI QURANI

MAKAMU WA RAIS ZANZIBAR ATOA ZAWADI KWA MSHINDI WA KUHIFADHI QURANI

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla, amewataka Wazee na Walimu wa Madrasa Nchini, kuwaendeleza kielimu katika fani mbali mbali za dini na dunia, Wanafunzi waliohifadhi Qurani, ili kupata radhi zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu. Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla ameyasema hayo katika hafla ya Mashindano Makuu ya kuhifadhi Quran ya Kitaifa

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Hemed Suleiman Abdulla akimkabidhi Mwanafunzi Fahad Haji shilingi Milioni Tano baada kupata nafasi kwa kwanza kwenye mashindano ya kuhifadhi Qurani hapo Mazizini Masjid Jamiuu Zinjibar.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla, amewataka Wazee na Walimu wa Madrasa Nchini, kuwaendeleza kielimu katika fani mbali mbali za dini na dunia, Wanafunzi waliohifadhi Qurani, ili kupata radhi zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu.

Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla ameyasema hayo katika hafla ya Mashindano Makuu ya kuhifadhi Quran ya Kitaifa Zanzibar ya juzuu 30 yaliyohitimishwa katika Masjid Jaamiu Zinjibaar, Mazizini Zanzibar.

Amesema kuwa wanafunzi waliopata fursa ya kuhifadhi Quran ni vyema kuandaliwa mazingira mazuri ya kielimu, ili wasiishie kushiriki mashindanoni na kupata zawadi, bali waandaliwe mfumo mzuri wa kuendelea na masomo akitolea mfano kujua tafsiri ya kile walichokihifadhi.

Akigusia suala la umuhimu wa kitabu cha Quran Mheshimiwa Hemed amesema ipo haja ya kuendelea kuisoma zaidi Quran hasa katika mwezi huu Mtukufu wa Ramadhan, ili kupata ujira mkubwa, akitolea mfano kuwa, mwenye kusoma quran, aajihakikishia uombezi siku ya kiama.

Amewausia  Wana Jumuiya na Walimu wa Vyuo vya Quran kwamba wasikate tamaa na mazingira magumu wanayofanyia Kazi kwani jukumu wanalolisimamia lina ujira mkubwa kwa Muumba wao ambaye hashindwi kuwashushia Rehema zake.

Mapema akitoa Taarifa ya Jumuiya ya kuhifadhi Quran Zanzibar Mwenyekiti wa Taasisi hiyo ya Kiislamu Mwanazuoni Sheikh Suleiman Omar {Maalim Sule} alisema Jumuiya hiyo iliyoasisiwa Mnamo Mwaka 1992 hivi sasa imeshatimiza miaka 28.

Maalim Suleiman alisema lengo la Jumuiya hiyo ni kusimamia ujenzi wa Maadili mema katika Kizazi cha Kiislamu katika kujikita zaidi kwenye Uhifadhi ya Kitabu Kitakatifu cha Quran ambapo kwa sasa zaidi ya Wanafunzi 300 wameshafanikiwa kukihifadhi moyoni Kitabu hicho.

Akitoa salamu Mmoja wa Waumini wanaoiunga mkono Jumuiya hiyo kwa kiwango kikubwa Mfanyabiashara Maarufu Nchini Sheikh Said Nasser Bopar alisema Waumini lazima washindane kwa nguvu na mali zao katika kuisimamia njia sahihi ya mwenyezi Mungu.

Matokeo ya Mashindano hayo ya kuhifadhi Quran yamemuwezesha Mwanafunzi Fahad Haji kushika nafasi ya kwanza kwa kupata alama 99 akizawadiwa shilingi Milioni 5,000,000/- na zawadi maalum.

Mshindi wa Pili alikuwa Mwanafunzi Abdull Nassir aliyepata alama 98 akikabidhiwa shilingi Milioni 4,000,000/- taslim wakati mshindi wa Tatu Shamis Maalim aliyepata alama 98 na kuzawadiwa shilingi Milioni 3,000,000/-.

Kwa upande wa Tashjii Tahqiq Mshindi wa kwanza alikuwa Mwanafunzi Rashid Hemed Rashid aliyeibuka na alama 100 na kuzawadiwa shilingi Milioni 2,500,000/-.

……………….

Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

25/04/2021.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »