KUANZISHWA KWA KIWANDA CHA KUSAFISHA MADINI CHA GGR KUTACHANGAMSHA UCHUMI WA GEITA-WAZIRI BITEKO.

KUANZISHWA KWA KIWANDA CHA KUSAFISHA MADINI CHA GGR KUTACHANGAMSHA UCHUMI WA GEITA-WAZIRI BITEKO.

Imeelezwa kuwa kuanzishwa kwa kiwanda cha Kusafisha Madinicha Mkoani Geita kitaongeza na kuchangamsha uchumi wa mkoana Taifa kwa ujumla wake.Waziri wa Madini Mhe Doto Biteko jana tarehe 8 Mei 2021 wakatiakiweka Jiwe la Msingi katika kiwanda cha kusafisha madini chaGGR akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Geita.Waziri Biteko amesema kuwa kiwanda hicho cha kisasa na

Waziri wa Madini Mhe Doto Biteko akiwa katika picha ya
pamoja na Viongozi wa Mkoa wa Geita pamoja na uongozi wa
kiwanda cha kusafisha dhahabu cha GGR mara baada ya kuweka
Jiwe la Msingi katika kiwanda hicho cha kusafisha madini cha GGR
wakati akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Geita, tarehe 8 Mei

2021.
Waziri wa Madini Mhe Doto Biteko akiweka Jiwe la
Msingi katika kiwanda cha kusafisha madini cha GGR wakati akiwa
katika ziara ya kikazi Mkoani Geita, tarehe 8 Mei 2021.
Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya kiwanda cha kusafisha
madini cha GGR Mhandisi Athuman Mfutakamba akisoma
taarifa mbele ya Waziri wa Madini Mhe Doto Biteko wakati akiwa
katika ziara ya kikazi Mkoani Geita, tarehe 8 Mei 2021.
Waziri wa Madini Mhe Doto Biteko akiwa ameambatana
na Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe Mhandisi Gabriel Robert akiweka
Jiwe la Msingi katika kiwanda cha kusafisha madini cha GGR
wakati akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Geita, tarehe 8 Mei
2021.
Waziri wa Madini Mhe Doto Biteko akisisitiza jambo
mara baada ya kuweka Jiwe la Msingi katika kiwanda cha
kusafisha madini cha GGR wakati akiwa katika ziara ya kikazi
Mkoani Geita, tarehe 8 Mei 2021.



Imeelezwa kuwa kuanzishwa kwa kiwanda cha Kusafisha Madini
cha Mkoani Geita kitaongeza na kuchangamsha uchumi wa mkoa
na Taifa kwa ujumla wake.
Waziri wa Madini Mhe Doto Biteko jana tarehe 8 Mei 2021 wakati
akiweka Jiwe la Msingi katika kiwanda cha kusafisha madini cha
GGR akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Geita.
Waziri Biteko amesema kuwa kiwanda hicho cha kisasa na cha
kwanza cha aina yake barani Afrika kimekusudia kuimarisha nyanja
za kusafisha dhababu nchini jambo litakaloimarisha soko la
uhakika la uuzaji wa madini na kuiwezesha Benki kuu kununua
madini yenyewe.
Amesema kuwa ni fahari kubwa katika sekta ya madini kwani
uwekezaji huo ni mkubwa na muhimu utakaokijibu ndoto za
serikali katika kuwakomboa wachimbaji wadogo wa madini.
Mhe Biteko amewaasa wachimbaji kuwa na ushirikiano na
kupendana kwani uchumi wa nchi hauwezi kuimarika kwa baadhi
ya wachimabji kuwachukia waliofanikiwa.
“Nasikitika kuna vijiwe vimegawanyika kazi yao kusuka majuku na
kuwachukia wengine waliofanikiwa, Ushindeni ubaya kwa wema,
aliyefanikiwa tumuombee Mungu amsogeze mbele” Amekaririwa
Waziri Biteko
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Gabriel
Robert amesema kuwa dhahabu inayouzwa katika mkoa huo
imeamsha ari kwa wawekezaji kuanza kuwekeza katika sekta
mbalimbali jambo linaloimarisha uchumi wa mkoa.
Amesema kuwa mkoa wa Geita pamoja na mambo mengine lakini
ni sehemu sahihi kwa ajili ya kuwekeza katika sekta ya madini.

Awali akisoma taarifa ya kiwanda cha kusafisha madini cha GGR
Kaimu Mkurugenzi wa Bodi Mhandisi Athuman Mfutakamba
amesema kuwa kiwanda hicho kilipewa leseni ya kusafisha
dhahabu No RFL 001/2019 iliyotolewa na Wizara ya Madini tarehe
16 Julai 2019 na kina uwezo wa kusafisha 400 kg kwa siku na
kufikia tani 200 kwa mwaka kwa kiwango cha juu kabisa na
kukidhi kufikia kiwango cha usafi wa asilimia 999.9 na 999.5
Amesema kampuni imejiimarisha ipasavyo kutekeleza wajibu huo
kwa kufunga vifaa/mashine za kusafisha dhahabu vya kisasa na
vyenye viwango vya hali ya juu vinavyokidhi viwango vya
kimataifa.

Na Mathias Canal, WazoHuru-Geita

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »