IKIWA NI MAADHIMISHO YA SIKU YA WAUGUZI DUNIANI, WAUGUZI WAKUMBUSHWA KUZINGATIA MAADILI YA KITAALUMA

IKIWA NI MAADHIMISHO YA SIKU YA WAUGUZI DUNIANI, WAUGUZI WAKUMBUSHWA KUZINGATIA MAADILI YA KITAALUMA

Na Barnabas Kisengi-Dodoma  TUME ya Haki za Binadamu na Utawala bora nchini imeungana na Waguzi wote Nchini kuadhimisha siku hiyo Duniani huku ikitoa wito kwa wauguzi kuzingatia maadili ya kitaaluma pamoja na kuwajibika licha kuwa na changamoto mbalimbali zinazowakabili. Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dodoma na Kamishina wa Tume hiyo,Dk Fatma Rashid Khalafan Kwaniaba ya

Na Barnabas Kisengi-Dodoma 

TUME ya Haki za Binadamu na Utawala bora nchini imeungana na Waguzi wote Nchini kuadhimisha siku hiyo Duniani huku ikitoa wito kwa wauguzi kuzingatia maadili ya kitaaluma pamoja na kuwajibika licha kuwa na changamoto mbalimbali zinazowakabili.

Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dodoma na Kamishina wa Tume hiyo,Dk Fatma Rashid Khalafan Kwaniaba ya Mwenyekiti wa Tume Jaji mstaafu Mathew Mwaimu wakati akizunghumza na wauguzi wa hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma mara baada ya kukabidhi zawadi   mbalimbali kwa wauguzi  ikiwemo sabuni na maji ya kunywa.

Aidha amewataka wauguzi kuhakikisha wanajiepusha na vitendo vinavyo weza kuwavunja moyo wauguzi na watoa huduma ya Afya ikiwemo lugha chafu na kujichukulia Sheria mkononi.

Sauti ya Kamishina wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala bora,Dk Fatma Rashid Khalafan

Katika hatua nyingine ameiomba Serrikali kuweka mazingira bora na salama ya kufanyia kazi ikiwemo kuboresha maslahi ya wauguzi.

Kwa upande wake  Stanley Mahundo ambaye ni Muuguzi mfawidhi Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma katika kurugenzi ya uuguzi amesema kama Hospitali wamejipanga kuwa dira katika utoaji wa huduma za Afya kwa wananchi,huku Grace Mlata ambaye ni Afisa Muuguzi Idara ya dharura amesema kuwa wamekuwa wakitoa huduma bila yakujali changamoto zinazowakabili.

Kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya wauguzi nchini ni muuguzi wauguzi ni sauti kuu inayoongoza katika Dira  ya afya.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »