VIJIJI 80 KUNUFAIKA NA UMEME WA REA MOROGORO

VIJIJI 80 KUNUFAIKA NA UMEME WA REA MOROGORO

NA MWANDISHI WETU -MOROGORO. JUMLA ya Vijiji 80 wilaya ya Morogoro vinatarajiwa kunufaika na mradi wa umeme wa Rea awamu ya tatu baada ya serikali kuviorodhesha vijiji hivyo kuingia kwenye mpango huo ili kuhakikisha kila kijiji kinakuwa na umeme wilayani hapo. Hayo yalisemwa na Kaimu Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO) wilaya ya Morogoro Hilda

NA MWANDISHI WETU -MOROGORO.

JUMLA ya Vijiji 80 wilaya ya Morogoro vinatarajiwa kunufaika na mradi wa umeme wa Rea awamu ya tatu baada ya serikali kuviorodhesha vijiji hivyo kuingia kwenye mpango huo ili kuhakikisha kila kijiji kinakuwa na umeme wilayani hapo.

Hayo yalisemwa na Kaimu Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO) wilaya ya Morogoro Hilda Luvuvu wakati akitoa taarifa kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Morogoro.

Hilda alisema vijiji ambavyo havina umeme katika wilaya hiyo vipo 80 na kwamba tayari maandalizi ya kupeleka umeme yameshaanza ambapo alisema kuwa muda wowote kuanzia sasa navyo vitakuwa na umeme”alisema Hilda.

Alisema wataalamu wa meme huo tayari wameshaanza hatua za awali za kuvikagua ambapo baada ya kukamilika kwa zoezi hilo vijiji vyote 150 katika wilaya hiyo vitakuwa na meme wa Rea hali itakayochochea maendeleo yao.

“Zoezi la kupeleka umeme kwenye vijiji ambavyo havina huduma hii ya nishati linakwenda vizuri na kwamba muda wowote kuanzia sasa vijiji vyote 150 katika halmashauri ya wilaya ya Morogoro vitakuwa na umeme wa Rea”alisema Hilda.

Hilda alisema kuwa kuwepo kwa umeme huo katika wilaya hiyo kutachochea ukuaji wa uchumi kwa wananchi hivyo Tanesco itahakikisha zoezi la kupeleka umeme kwenye vijiji ambavyo hajipajapa umeme linafanyika kwa haraka zaidi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya hiyo ya Morogoro Lucas Lemomo alisema kuwa wananchi wa vijiji hivyo wapo tayari kuona umeme huo unawafikia kwani wanaamni itakuwa ni moja ya njia ya kupata maendeleo.

Alisema kuwepo kwa umeme huo wa Rea katika vijiji vyote katika wilaya hiyo, Halmashauri yake itakuwa ma maendeleo mengi ya kiuchumi kwani watu wengi watuvutiwa kufika katika wilaya hiyo kwa ajili ya kuwezeka viwanda vingi sana.

“Wilaya yetu hii ni maarufu kwa kilimo cha mazao ya aina mbalimbali hivyo kitendo cha kuwa na umeme kutasaidia kuwavuta wawekezaji kuja hapa kwa ajili ya kuwekeza viwanda vya uchakataji wa mazao ya wakulima”alisema Lemomo.

alisema kitendo cha uchakataji wa mazao kutaomgeza thamani yake hivyo kufanya uchumi wa wakulima ambao ndiyo walishaji wakubwa wa mazao hayo kuwa imara na pia kutasaidia sana kuongeza mapato ya Halimashauri hiyo kwa ujumla wake.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya hiyo Rehema Bwasi amewataka wananchi wote kuepuka kuwa chanzo cha kukwamisha mradi huo kwani mradi huo wa Rea utakuwa chachu kubwa ya maendeleo kwa kila kijiji.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »