WAZIRI MKUU AKARIBISHA WAWEKEZAJI KUTOKA CHINA.
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema hadi kufikia sasa China imewekeza zaidi ya dola bilioni 10 katika maeneo mbalimbali nchini na ametumia fursa hiyo kuwakaribisha wawekezaji wengine zaidi. Amesema kuwa takwimu za Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) zinaonesha kuwa kuna zaidi ya miradi 1,134 ambayo imesajiliwa kutoka makampuni ya China na hivyo kuchangia ajira kwa Watanzania.