Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe Othman amezindua Jengo la SAMIA SULUHU HASSAN MBAGALA HOSPITAL.

Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe Othman amezindua Jengo la SAMIA SULUHU HASSAN MBAGALA HOSPITAL.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Othman Masoud Othman, Leo Alhamis Aprili 25, 2024, ameshiriki akiwa Mgeni Rasmi katika Uzinduzi wa Jengo la Ghorofa Sita (6) la ‘SAMIA SULUHU HASSAN MBAGALA HOSPITAL’, lililopo Mbagala Rangi Tatu, Manispaa ya Temeke Mkoa wa Dar es Salaam. Jengo hilo ambalo ni miongoni mwa Miradi ya Tawala

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Othman Masoud Othman, Leo Alhamis Aprili 25, 2024, ameshiriki akiwa Mgeni Rasmi katika Uzinduzi wa Jengo la Ghorofa Sita (6) la ‘SAMIA SULUHU HASSAN MBAGALA HOSPITAL’, lililopo Mbagala Rangi Tatu, Manispaa ya Temeke Mkoa wa Dar es Salaam.

Jengo hilo ambalo ni miongoni mwa Miradi ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), katika Halmashauri ya Wilaya ya Temeke, na ambalo pia linatrajiwa kukamilika ifikapo Mwezi wa Juni, Mwaka 2025, limezinduliwa, ikiwa ni Sehemu ya Shamra-shamra za Kutimu Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Mheshimiwa Othman aliyeambatana na Mke wake, Mama Zainab Kombo Shaib, amewasili Jijini Dar es Salaam, kwa Ziara ya Siku Moja ikiambatana na Ufunguzi wa Majengo ya Serikali, na pia kuhudhuria Kilele cha Maadhimisho ya Miaka Sitini (60) ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, yanayofanyika Kesho, Aprili 26.

Viongozi mbali mbali wa Serikali, Vyama vya Siasa, Wakurugenzi, Wauguzi wa Afya, Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama na Madiwani, wamehudhuria katika Uzinduzi huo, wakiwemo; Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Dkt. Omar Dadi Shajak; Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Ndg. Sixtus Mapunda; na Mstahiki Meya wa Temeke, Ndg. Abdalla Mtinika.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Translate »