Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk.Hussein Ali Mwinyi ameshiriki Maziko ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kwahani Zanzibar Mhe. Ahmada Yahya Abdulwakil aliyezikwa kijijini kwake Muyuni Mkoa wa Kusini Unguja tarehe: 09 Aprili 2024.
Mke wa Rais wa Zanzibar, Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) Mhe.Mama Mariam Mwinyi ametoa wito kwa Waumini wa Dini ya Kiislamu kuendelea kutenda mema , kuombeana baada ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na kuendelea kuwasaidia watu wenye mahitaji maalumu. Mama Mariam Mwinyi amesema hayo alipotoa