Mke wa Rais Mama Mariam Mwinyi amewataka Waumini wa Dini ya Kiislamu kuendelea kutenda mema.

Mke wa Rais Mama Mariam Mwinyi amewataka Waumini wa Dini ya Kiislamu kuendelea kutenda mema.

Mke wa Rais wa Zanzibar, Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) Mhe.Mama Mariam Mwinyi ametoa wito kwa Waumini wa Dini ya Kiislamu kuendelea kutenda mema , kuombeana baada ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na kuendelea kuwasaidia watu wenye mahitaji maalumu. Mama Mariam Mwinyi amesema hayo alipotoa

Mke wa Rais wa Zanzibar, Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) Mhe.Mama Mariam Mwinyi ametoa wito kwa Waumini wa Dini ya Kiislamu kuendelea kutenda mema , kuombeana baada ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na kuendelea kuwasaidia watu wenye mahitaji maalumu.

Mama Mariam Mwinyi amesema hayo alipotoa zawadi za mkono wa Eid alipotembelea vituo mbalimbali vya kuwalea Wazee na Watoto ikiwemo kituo cha kulea Watoto ZASO Fuoni Mambosasa, kituo cha Wazee Welezo , kituo cha Wazee Sebleni , kituo cha Watoto SOS na kituo cha Watoto Mazizini , Mkoa wa Mjini Magharibi tarehe: 10 Aprili 2024.

Aidha Mama Mariam Mwinyi amesema ni wajibu kuwalea, kuwatembelea na kuwaenzi Wazee kufanya hivyo ni baraka kubwa sana.

Halikadhalika Mama Mariam Mwinyi ameeleza kuwa Serikali itaendelea kuwasaidia Wazee na kuwajali.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »