Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba alipokuwa akiwasilisha Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka 2022/2023, Bungeni, Dodoma tarehe 14 Juni, 2022. Rais Samia amefuatilia hotuba hiyo ya Bunge wakati akiwa Muscat nchini Oman.READ MORE
Mtendaji Mkuu wa klabu ya Simba Sc Barbara Gonzalez akiongozana na msanifu majengo (architect) wamekagua mipaka ya eneo la Simba,Bunju jijini Dar es salaam ambalo litatumika kwenye ujenzi wa kiwanja Mo simba arena studium, zikiwa zimebaki siku chache kabla ya Bodi ya Wakurugenzi kukutana ili kupitisha mkandarasi ambaye atajenga.
Leo tumekabidhiwa Tuzo ya Klabu Bora kwenye Mitandao ya Kijamii Tanzania ambayo imetolewa na kampuni ya Serengeti Bytes. Tumeshinda tuzo hii baada ya kuvishinda kura vilabu vya Azam FC, Mbeya City, Ruvu Shooting na Yanga SC.