SIMULIZI: MAMA WA MIAKA 41 ABAKWA NA WATU TISA MVOMERO

SIMULIZI: MAMA WA MIAKA 41 ABAKWA NA WATU TISA MVOMERO

NA MWANDISHI WETU- MOROGORO KATIKA hali isiyo ya kawaida mama (41) ambaye jina lake limehifadhiwa amejikuta akiwa wakati mguu baada ya kufanyiwa kitendo cha ukatili wa kijinsia kwa kubakwa na vijana 9 wanaodaiwa kuwa ni jamii ya kimasai katika kijiji cha Mtakuja kata ya dakawa wilayani Mvomero Akisimulia madhira yaliyomkuta mama huyo alisema kuwa siku ya


NA MWANDISHI WETU- MOROGORO

KATIKA hali isiyo ya kawaida mama (41) ambaye jina lake limehifadhiwa amejikuta akiwa wakati mguu baada ya kufanyiwa kitendo cha ukatili wa kijinsia kwa kubakwa na vijana 9 wanaodaiwa kuwa ni jamii ya kimasai katika kijiji cha Mtakuja kata ya dakawa wilayani Mvomero

Akisimulia madhira yaliyomkuta mama huyo alisema kuwa siku ya tukio april 13 wak huu alikuwa na mume wake wakitoka dukani kufata mahitaji majira ya saa moja usiku ndipo walipovamiwa na kundi hilo la wamasai

Alisema vijana hao walianza kwa kumshambuliwa na mume wake kwa fimbo na rungu ambapo licha ya kujaribu kujitetea lakini walizidiwa nguvu na ndipo vijana hao wakafanya kitendo hicho kwa zaidi ya masaa manne.

“wakatu tunatoka dukani tulipofika karibu na uwanja wa pria ndio vijana hao wakatuvaia wakapiga ue wangu na fibo wakanikaata na ii wakanipiga na rungu kiunoni wakanilaza chini na kunivua nguzangu za ndani kasha wakafanya kitendo chao huku wakipokezana” alisema  

Aliongeza baada ya muda mrefu kupita aliwasikia vijana hao wakipigia simu mwenzao ili ajiunge nao ambapo naye baada ya kufika aliendelea kufanya kiteno hicho bila ya kujali kama anamfahamu mama huyo

Aliendelea kwa kusema kwasasa anaishi kwa wasiwasi na kulazimika kujificha ili kulinda uhai wake baada ya kupokea vitisho vya aina mbalimbali huku akidai baadhi ya wahusika hao bado wanaendelea kuonekana mtaani licha ya kufahamika hadi majina yao

“walipoaliza kufanya kitendo chao pale uwanjani walipigia wenzao abaye  ii nafahau naye akaja wakanitoa uwanjani wakanipeleka karibu na kijijini kuna kaburi lipo njiani wakarudia kufanya kiteno kile hata nilipojaribu kutaja jina la kijana ninaye fahau ndipo wakataka kunichoa na kisu lakini huyo kijana akawazuia” alisema

Kilio cha mama huyu kinafika mezani kwa mkuu wa wilaya ya Mvomero Albinus Mgonya akiwa katika kikao na wadau mbalimbali ambapo akataka kupata maelezo ya hatua zilizochukuliwa kutoka kwa mkuu wa polisi wilaya ya Mvomero

Sospeter Kungura ni mkuu wa polisi wilaya ya Mvomero alisema awali walikuwa wanawashikiria watuhumiwa watatu ambapo kati yao wawili waliachiliwa kwa dhamana na mtuhumiwa moja bado anashikiliwa na jeshi hilo

Alisema mpaka sasa hatua mbalimbali zimechukuliwa ikiwemo kufikisha jarada kwa mkuu wa mashtaka mkoa wa Morogoro kwaajili ya kufikisha mtuhumiwa mahakani wakati uchunguzi ukiendelea kubaini wengine wanaohusika

“sio kweli kwamba tunasubiri mpaka watuhumiwa wote tisa wakamatwe ndio tufungue kesi, tayari jarada lilishapelekwa ofisi ya mashtaka mkoa na limesharudi, lakini huwa tunakabiliwa na changamoto ya kukosa ushirikiano kwa wahanga ndio maana lawama zote zinaruda kwa jeshi la polisi hata kaa wadau wengine waetukwamisha” alisema Kungura

Hata hivyo mkuu wa wilaya alionesha kutoridhishwa  na hatua zilizochukuliwa na kulitaka jeshi la polisi wilayani humo kuwakamata watuhumiwa wote tisa waliopo mtaani ndini ya muda mfupi ili hatua ziweze kuchukuliwa

Alisema haiwezekani tukio hilo litokee tangu april 13 mwaka huu lakini jeshi hilo linazungusha upelelezi wa kesi hiyo wakati taarifa za wahusika zinajulikana huku wengine wakiendelea kuonekana mtaani wakiendelea na maisha ya kawaida

“kitendo hiki kama serikali hatuwezi kukivumilia hata kidogo OCD na timu yako nataka ndani ya siku 30 watuhumiwa wote wawe wameshakamatwa na uniletee ofisini kwangu taarifa ya kukatwa kwao kwasababu watu wanajulikana kwa majina lakini kesi haiendelei na mama wa watu anaendelea kuteseka” alisea Mgonya

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »