Radi yauwa Kigoma.

Watu wawili wamefariki duniani baada ya kupigwa na radi iliyoambatana na mvua kubwa iliyonyesha siku ya jana katika Manispaa ya Kigoma Ujiji Mkoani Kigoma. Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma ACP James Manyama amethibitisha vifo hivyo na kueleza kuwa mmoja kati ya waliokutwa na mauti ni Kijana aliyefahamika kwa jina la Yassin Khalifan mwenye umri wa

Kamanda wa Polisi Mkoani Kigoma, ACP James Manyama.

Watu wawili wamefariki duniani baada ya kupigwa na radi iliyoambatana na mvua kubwa iliyonyesha siku ya jana katika Manispaa ya Kigoma Ujiji Mkoani Kigoma.

Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma ACP James Manyama amethibitisha vifo hivyo na kueleza kuwa mmoja kati ya waliokutwa na mauti ni Kijana aliyefahamika kwa jina la Yassin Khalifan mwenye umri wa miaka 18 mkazi wa Mtaa wa Gezaulole Kata ya Gungu Mkoani Kigoma.

Katika tukio lingine Kamanda Manyama amesema mvua hiyo imesababisha pia kifo cha mtoto anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 10 aliyekutwa amefariki baada ya kusombwa na maji katika Kata ya Kibirizi Manispaa ya Kigoma ujiji.

Kamanda Manyama ameeleza kuwa mvua hiyo iliyokuwa inaambatana na radi imewajeruhi wanafunzi watatu wa Shule ya Sekondari Jihad ambao wamepelekwa hospitali kwa matibabu zaidi

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »