RAIS DKT. MWINYI AMEWATAKA WAZANZIBARI KUACHA TABIA YA “MUHALI”

RAIS DKT. MWINYI AMEWATAKA WAZANZIBARI KUACHA TABIA YA “MUHALI”

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ameitaka jamii ya Wazanzibari kuacha tabia ya ”muhali” na kuripoti matukio ya vitendo vya udhalilishaji katika vyombo vya sheria huku akilitaka jeshi la Polisi kuacha kufanya usuluhishi wa matukio hayo. Akizungumza na wananchi pamoja na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi wa Mkoa

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ameitaka jamii ya Wazanzibari kuacha tabia ya ”muhali” na kuripoti matukio ya vitendo vya udhalilishaji katika vyombo vya sheria huku akilitaka jeshi la Polisi kuacha kufanya usuluhishi wa matukio hayo.

Akizungumza na wananchi pamoja na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi wa Mkoa wa Mjini Kichama  hapo Makao Makuu ya Chama hicho Mkoa Amani, katika ziara ya kuwashukuru, alisema bado hajaridhishwa na utendaji wa jeshi la Polisi katika kushughulikia kesi za udhalilishaji wa kijinsia.

Rais Dk. Mwinyi ambaye pia, ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) alisema yapo malalamiko kutoka kwa jamii kwamba jeshi la Polisi limekuwa likifanya upatanishi wa kusuluhisha wa kesi hizo katika vituo vya Polisi na kumalizana kienyeji.

Alifahamisha hizo sio kazi za jeshi la Polisi kwa mujibu wa sheria  ambapo wanatakiwa kuhakikisha wanatayarisha kesi kwa kufanya upelelezi na kuzipeleka mbele kwa hatua nyengine.

Hivyo, Rais Dk. Mwinyi alitumia fursa hiyo kuwapongeza Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa kufanya marekebisho mazuri katika sheria za udhalilishaji ambapo mtuhumiwa wa makosa hayo atakuwa akinyimwa  dhamana.

”Nilikutana na viongozi wa jeshi la Polisi,mkurugenzi wa mashtaka pamoja na mahakama na kuwataka wakutane na kuweka utaratibu mzuri utakaohakikisha kesi hizo zinasikilizwa haraka ili jamii iondokane na malalamiko”alisema.

Rais Dk. Mwinyi aliwapongeza Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa kufanya marekebisho mazuri katika sheria ya udhalilishaji ambapo mtuhumiwa wa makosa hayo atakuwa akinyimwa  dhamana.

”Nimemtaka jaji mkuu sheria itekelezwa wanaofanya vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia kwanza wanyimwe dhamana huku shauri lao likiendelea”alisisitiza Dk. Mwinyi.

Aidha, Rais Dk. Mwinyi aliwaeleza wananchi na wanachama wa chama cha CCM Mkoa wa Mjini kwamba katika kipindi cha miezi sita ya uongozi wake amefanikiwa kujenga misingi ya maridhiano ya kisiasa ya serikali ya umoja wa kitaifa.

Alisema kuwepo kwa serikali ya umoja wa kitaifa kumefunguwa milango ya maelewano yaa kisiasa na kijamii na kuondokana na chuki huku zikiwemo  kila aina ya dalili za matumaini yenye kheri.

Aliwajulisha wananchi kwamba maandalizi ya ujenzi wa bandari za kisasa yenye urefu wa kilomita sita huko Mangapwani na Bumbwini upo katika hatua za mwisho ambao ni sehemu ya matarajio makubwa ya kutengeneza ajira nyingi.

”Hapa wananchi na wanachama wengi wamezungumzia suala la serikali kuajiri vijana waliomaliza masomo yao…si kweli serikali haiwezi kuajiri vijana wote hao lakini tunatengeneza mazingira ya ajira kwa kujenga miundo mbinu ya bandari na viwanda”alisema.

Rais Dk. Mwinyi alieleza nama Serikali yake inavyokusudia kutafuta eneo mbadala kwa ajili ya kuwashughulikia wale walioathirika na dawa za kulevya kwani katika eneo la Hospitali ya Kidongochekundu mazingira yake hayaridhishi.

Alieleza hatua zitakazochukuliwa katika kuhakikisha wazee wanaangaliwa katika suala zima la pencheni zao pamoja na huduma wanazostahiki zikiwemo huduma za afya.

Nae Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Aballa Juma Mabodi aliwataka watendaji wa chama hicho wakiwemo Makatibu kujipanga kwa ajili ya kutekeleza Ilani ya Chama hicho kwa kufuatilia ahadi zote za Serikali katika kipindi cha kampeni za uchaguzi mkuu.

”Nawataka watendaji wa chama sasa mjipange vizuri kufanya kazi zenu ikiwemo kuifuatilia serikali utendaji wake unaotokana na ahadi katika kipindi cha uchaguzi mkuu”alisema.

Mabodi alikikea tabia ya baadhi ya wanachama wa chama hicho ya kuanza kampeni za uchaguzi wa chama hicho kabla ya muda kufika hapo mwakani.

Katika risala yao viongozi hao wa CCM wa Mkoa wa Mjini walieleza mafanikio ya Chama hicho waliyoyapata katika uchaguzi uliopita sambamba na kumpongeza Rais Dk. Mwinyi kwa juhudi zake za uongozi pamoja na kumpongeza kwa kulivalia njuga suala la waathirika wa “Masterlife” ambalo limewaathiri wananchi wengi ambao ni wakaazi wa Mjini.

Mapema Rais Dk. Mwinyi aliwapa nafasi viongozi hao na wanaCCM ya kuzungumza pamoja na kueleza changamoto zinazowakabili huku wakitumia fursa hiyo kwa kupambana na ufisadi na ubadhirifu wa mali ya umma.

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822
E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »