WIZARA YA KATIBA YAJA NA SHERIA KWA MAHABUSU

MOROGORO. SERIKALI kupitia Wizara ya Katiba na Sheria imetunga sheria mpya ya usuluhishi,upatanishi,majadiliano na maridhiano itakayotumika katika utatuzi wa migogoro ili kuhakikisha wanaunga mkono juhudi za wadau mbalimbali. Hayo yalisemwa juzi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Amon Mpanju mkoani hapa ambapo serikali inaunga mkono juhudi za wadau katika suala zima la kupunguza

MOROGORO.

SERIKALI kupitia Wizara ya Katiba na Sheria imetunga sheria mpya ya usuluhishi,upatanishi,majadiliano na maridhiano itakayotumika katika utatuzi wa migogoro ili kuhakikisha wanaunga mkono juhudi za wadau mbalimbali.

Hayo yalisemwa juzi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Amon Mpanju mkoani hapa ambapo serikali inaunga mkono juhudi za wadau katika suala zima la kupunguza msongamono wa wafungwa maabusu ili kupunguza gharama.

 Mpanju alisema kuwa Wizara yake inaunga mkono juhudi zote zinazofanywa na baadhi asasi zisizo za kiserikali za kupunguza msongamano wa mahabusu vizuizini wanaoisababishia serikali kutumia gharama kubwa ya kuwahudumia watuhumiwa.

“Tumeamua kutunga sheria mpya itakatosaidia kupata usuluhisi,upatanishi,majadiliano na maridhiano ili kupunguza watuhumiwa mahabusu  na pia kupunguza gharama ya kuwahudumia”alisema Mpanju.

Naibu Katibu Mkuu huyo alikiri kuwepo kwa ufinyu wa magereza nchini kwa sababu baadhi ya magereza zilijengwa kipindi cha ukoloni na kwamba serikali imeanza mchakato wa kupunguza msongamano huo mahabusu magerezani.

Alieleza tayari Tanzania inatumia tehama katika utoaji haki hasa mahakamani hivyo kufanya baadhi ya kesi kusomwa na kusikilizwa kwa wakati na kupunguza mrundikano wa kesi hali iliyonguza changamoto ya kusafirisha mahabusu.

Mkurugenzi wa Asasi isiyokuwa ya kiserikali ya Wasaidizi wa Kisheria magerezani na vituo vya polisi (ENVIROCARE) Loyce Lema alisema kuwa tayari asasi hiyo inatekeleza mradi wa kupunguza msongamano huo nchini.

Mukurengi huyo alisema hadi sasa tayari mradi huo umefanikiwa kuyafikia magereza 26,vituo vya polisi 94 katika mikoa 14 ya Tanzania Bara lengo kuu likiwa kufanikisha suala la kupunguza msongamano wa mahabusu vizuizini.

“ Tulianza kutoa mafunzo ya msaada wa kisheria kwa baadhi ya maafisa wa jeshi la polisi,magereza,mahakama na viongozi wa serikali za mtaa ambao wamekuwa wakitoa ushirikiano kusaidia kupatikana kwa haki kwa mahabusu”alisema Loyce.

Kwa upande wake Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Morogoro Fortunatus Muslim kwa niaba ya Mkuu wa jeshi hilo nchini alizitaka asasi hizo kutoa mafunzo zaidi ya kisheria kwa maafisa wengi wa jeshi hilo la polisi ili kuongeza ufanisi.

Kamanda Muslim alizitaka asasi hizo kutoa mafunzo ya kisheria kwa jeshi hilo nchini ili kuhakikisha kunakuwa na wigo mpana wa uelewa wa sheria na haki za binadamu kwa mahabusu kitendo kitakachosaidia kupunguza mlundikano wa maabusu.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »