IDADI YA WANAWAKE KUTELEKEZWA NA WATOTO YAONGEZEKA PWANI

IDADI YA WANAWAKE KUTELEKEZWA NA WATOTO YAONGEZEKA PWANI

Mkuu wa Dawati la jinsia mkoa Pwani Inspekta Hawa Juma amesema kumekuwa na ongezeko la kutelekezwa kwa mama na mtoto katika mkoa huo. Akizungumza na J five mjini kibaha mkoani Pwani Inspekta Hawa amesema wengi wa wanawake hao wanaotekeleza ni wamama wadogo ambao hupewa ujauzito chini ya miaka 18 ambao walibakwa na bodaboda, madereva wa

Mkuu wa Dawati la jinsia mkoa Pwani Inspekta Hawa Juma amesema kumekuwa na ongezeko la kutelekezwa kwa mama na mtoto katika mkoa huo.

Akizungumza na J five mjini kibaha mkoani Pwani Inspekta Hawa amesema wengi wa wanawake hao wanaotekeleza ni wamama wadogo ambao hupewa ujauzito chini ya miaka 18 ambao walibakwa na bodaboda, madereva wa malori, vijana vijiweni na makundi mengine ya wanaume ikasababisha ujauzito.

“Mama wadogo hao wakakatishwa masomo yao wakakaa nyumbani wanalea watoto lakini kwasababu hao wababa waliwabaka kwania ya kutimiza tu hamu yao au malengo yao linapokuja suala la ujauzito na kulea watoto hao wababa wanakimbilia na kuwaacha mama na watoto bila huduma” alisema inspekta Hawa.

Aliongeza kuwa “Hawa wamama ambao ni wadogo wanabaki kutaabika na malezi ya watoto kwahiyo hapo ndipo tunaona kuna ongezeko la wamama kutelekezewa watoto”

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »