Uharibifu wa mazingira walisukuma shirika la TFCG kuanza kutoa elimu ya mazingira

Uharibifu wa mazingira walisukuma shirika la TFCG kuanza kutoa elimu ya mazingira

NA DOTTO KWILASA,DODOMA. KATIKA kuunga mkono juhudi za Serikali kuhusu uhifadhi wa Mazingira,Shirika lisilo la kiserikali la uhifadhi wa misitu tanzania(TFCG)kimetoa kipaumbele cha kupeleka elimu ya mazingira kwa shule za msingi Tanzania kwa kuanza na Maeneo ya Wilaya ya Mufindi-Iringa,Kilosa na Mvomelo -Morogoro Pamoja na Morogoro Vijijini.Hayo yamebainishwa hivi karibuni Jijini hapa na Afisa Elimu 

NA DOTTO KWILASA,DODOMA.


KATIKA kuunga mkono juhudi za Serikali kuhusu uhifadhi wa Mazingira,Shirika lisilo la kiserikali la uhifadhi wa misitu tanzania(TFCG)kimetoa kipaumbele cha kupeleka elimu ya mazingira kwa shule za msingi Tanzania kwa kuanza na Maeneo ya Wilaya ya Mufindi-Iringa,Kilosa na Mvomelo -Morogoro Pamoja na Morogoro Vijijini.
Hayo yamebainishwa hivi karibuni Jijini hapa na Afisa Elimu  Mazingira Msaidizi wa TFCG Francis Fawel  Katika mahojiano maalum na gazeti hili  wakati wa wiki ya mazingira iliyolenga kuukumbusha Umma  umuhimu wa mazingira .


Akifafanua zaidi kuhusu hilo alieleza kuwa kupitia mbinu hiyo wanafunzi watajenga uelewa wa namna ya kuhifadhi mazingira na kuwa mabalozi kwa jamii kuhusu namna ya kuenzi na kuyaishi mazingira ikiwa ni Pamoja na kutumia rasilimali zipatikanazo katika njia endelevu na zenye uwiano.
Licha ya hayo katika muktadha wa mazingira wanafunzi hupata nafasi ya kujadiliana mambo ya mazingira, kutengeneza mawazo yao, kutoka na kufanya kazi nje ya darasa. “Tunawashirikisha wanafunzi kupitia klabu ya mazingira  katika ili kufanya mafunzo yaendane na welewa wa wanafunzi na vilevile yawe na kichocheo cha kubadilisha mazingira ya shule,ni muhimu kwa wanafunzi kujifunza ili kuwaelimisha wengine,”alisema.


Pamoja na hayo amesema kwa kuzingatia umuhimu wa mazingira kuanzia shuleni,TFCG imedhamini miradi midogo midogo ya ufugaji Nyuki,Bustani na kwamba kwa kufanya hivyo jamii itapata ujumbe wa kuendelea kulia makazo suala la mazingira.
Naye Afisa sera na majadiliano wa Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania (MJUMITA) Elda Fundi alieleza kuwa kuna umuhimu wa kuendelea kupambana kwa bidii na kuhakikisha mazingira yanalindwa.


Amesema,uanzishwaji wa kanuni zinazokinzana na usimamizi wa Mazingira  umesababisha dhana ya Usimamizi shirikishi wa Misitu (USMJ)kushindwa kutekelezeka kama ilivyokusudiwa.
Akifafanua hilo amesema,Kutokana na Sheria hizo kumesababisha mauzo ya biashara ya mazao ya misitu kwenye usimamizi shirikishi wa misitu kushika na kusababisha Serikali za Vijiji kukosa mapato kutoka kwenye hifadhi za misitu ya vijiji hali inayosababisha kukwama kwa baadhi ya miradi ya Maendeleo ya Jamii Katika ngazi za Vijiji.
“Tangu awali Serikali ya Tanzania ilitoa Sera,Sheria na miongozo wezeshi kwa jamii kusimamia misitu iliyoko kwenye ardhi ya vijiji kwa njia endelevu chini ya Taasisi huru za Serikali ya Kijiji na kupelekea jamii ya eneo husika kunufaika na usimamizi endelevu wa misitu hiyo,”alisema na kuongeza;
Mabadiliko yaliyofanywa hivi karibuni na kanuni za misitu GN 417 ya Mwaka 2019 umeifanya dhana ya usimamizi shirikishi wa misitu kushindwa kutekelezeka kama ilivyokusudiwa,”alisema.


Pamoja na mambo mengine Fundi amesema kwa kuwa sasa Usimamizi huo shirikishi hautoi faida ya kiuchumi kwa jamii inayosimamia misitu hiyo,Kuna hatari kubwa ya misitu iliyokuwa ikilindwa na watu wa eneo hilo kwa miaka 5-7 iliyopita kubadilishwa na kuwa mashamba.
Kutokana na hali hiyo aliishauri Serikali kupitia Wizara ya Mali asili na Utalii kuona haja ya kutoa ufafanuzi juu ya matumizi ya kanuni hizo hususani katika misitu ya vijiji/jamii.


Mbali na hayo alishauri sera,Sheria na miongozo ya misitu kuendelea kutambua haki za jamii za kumiliki,kusimamia na kutumia misitu na rasilimali za misitu kwa njia endelevu.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »