SERIKALI imeazimia kuimarisha Taasisi zote za utoaji Haki hasa Mahakama .

SERIKALI imeazimia kuimarisha Taasisi zote za  utoaji Haki hasa Mahakama .

SERIKALI imesema imeazimia kuendelea kuimarisha Taasisi zote za  utoaji Haki hasa Mahakama pamoja na kutatua changamoto  zinazo ikabili sekta hiyo  hasa uhaba wa watumishi huku akiwataka Wanasheria wote wa Umma nchini kuhakikisha wanafanya  mashauriano na Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kabla ya kuanza kesi ili kushinda. Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dodoma na   Waziri wa Katiba na Sheria Profesa

SERIKALI imesema imeazimia kuendelea kuimarisha Taasisi zote za  utoaji Haki hasa Mahakama pamoja na kutatua changamoto  zinazo ikabili sekta hiyo  hasa uhaba wa watumishi huku akiwataka Wanasheria wote wa Umma nchini kuhakikisha wanafanya  mashauriano na Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kabla ya kuanza kesi ili kushinda.

Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dodoma na   Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Paramagamba  Kabudi wakati akifungua mkutano wa kwanza wa Watumishi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali nakusema Serikali itahakikisha inazifanyia kazi changamoto zote.

Aidha amesema katika kufanya mashauri yote kupitia ofisi ya wakili wa Serikali itasaidia wao kujipanga kisheroia katika mashauri yao.

Hata hivyo ametaka  kuona umuhimuwa matumizi ya lugha ya Kiswahili  katika mahakama kwakuweka istilahi na misamiati ya kisheria katika suala zima la uendeshaji kesi.

Wakili Mkuu wa Serikali,Gabriel Malata.

Kwa upande wake Wakili Mkuu wa Serikali,Gabriel Malata ameiomba Serikali kupitia Wizara ya Katiba na Sheria kuwapa mafunzo ili kuwajengea uwezo katika uendeshaji wa madai ya Gesi na Madini katika kuelekea uchumi wa Viwanda kutokana na wanasheria wengi kutokuwa na uelewa wa masuala hayo.

Sambamba na hilo ameeleza changamoto mbalimbali ikiwemo uhaba wa watumishi na Vitendea kazi ikiwemo watumishi walipo ni 143 huku mahitaji ni 312.

Na Barnabas kisengi Dodoma 

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »