Katibu Mkuu UVCCM amewataka Vijana kutumia mitandao ya kijami kupata kipato na si kudhalilisha utu wa viongozi, Chama na Taifa.

Katibu Mkuu UVCCM amewataka Vijana kutumia mitandao ya  kijami kupata kipato na si kudhalilisha utu wa viongozi, Chama na Taifa.

KATIBU Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha  Mapinduzi  (UVCCM) Kenani Kihongosi amewataka Vijana   kutumia mitandao ya  kijami kwa kupata kipato na kupashana habari  zenye  tija na si kudhalilisha utu wa viongozi Chama na Taifa.Ameyasema hayo leo Jijini hapa wakati akizungumza na Vijana wa umoja huo kwenye hafla fupi ya kukaribishwa kwake Makao Makuu

KATIBU Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha  Mapinduzi  (UVCCM) Kenani Kihongosi amewataka Vijana   kutumia mitandao ya  kijami kwa kupata kipato na kupashana habari  zenye  tija na si kudhalilisha utu wa viongozi Chama na Taifa.
Ameyasema hayo leo Jijini hapa wakati akizungumza na Vijana wa umoja huo kwenye hafla fupi ya kukaribishwa kwake Makao Makuu mara baada ya kuteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan kushika wadhifa huo hivi karibuni.
Kihongosi amesema Vijana Wengi hapa nchini wamekuwa wakijihusisha vibaya na mitandao ya kijamii kwa viongozi ,kudhalilishana ,kudhihaki Jambo ambalo ni kinyume na ukiukwaji wa sheria za chama na Taifa .
“Katika mitandao Kuna mijadala isiyo na tija kila mmoja atumie mitandao vizuri   tutumie mitandao kwa kupata kipato ndugu zangu na kupashana habari na si vinginevyo na niwasihi chama hakitasita kuwachukulia hatua Kali wale watakaokwenda kinyume na maadili,
“Badala ya kushinda kwenye mitandao bila tija niwasihi kutumia mitandao hiyo kutangaza miradi ya Serikali inayotekelezwa kwenye eneo unaloishi huku ukitafuta fursa za ajira Jambo ambalo litawafanya kuchochea maendeleo kwa jamii”amesema Kihongosi
Aidha ameutaka umoja huo kuepuka  migogoro Katika kazi hususani majungu,dharau na ugomvi ambayo yamekuwa kero kubwa bali wadumishe umoja , upendo na mshikamano viwe nguzo ili kulitumikia Taifa .
Katika hatua nyingine amewakemea vikali baadhi ya Vijana ambao wamekuwa msitari wa mbele kuwabeba na kuanza kuwanadi wagombea kabla ya muda wake Jambo ambalo sio sahihi na utaratibu wa chama Cha Mapinduzi CCM na kudai wasubiri mwakani ili waanze kampeni.
Vilevile  amewataka viongozi  wa umoja huo kutembelea sehemu zenye changamoto za Vijana Kama wafanyakazi wa hotelini,dereva bajaji,bodaboda, na mama ntilie ,machinga ,mafundi ujenzi,umeme,wakulima,wavuvi,pamoja na makundi yote  ili kujua changamoto wanazokumbana nazo na kuzifikisha kwenye chama ili zipatiwe ufumbuzi  kwa maslahi ya Serikali.
“Niwatake viongozi huko Mikoani na Wilaya zote kufika kwenye Halmashauri za Wilaya  muongee na wakurugenzi namna ya kupewa zile asilimia zinazotengwa kuwakopesha Vijana bila riba ili waweze kufanya biashara mbalimbali na kujikwamua kiuchumi kwani fedha hizo zimekuwa zikitumika kwa watu wengine”amesema Kiongosi.
Awali akizungumza Katika hafla hiyo Naibu waziri Ofsi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye Ulemavu ,Ummy Nderiananga amewataka Vijana kuiga mfano wa Katibu Mkuu huyo  kuwa na nidhamu ,kujituma Katika Chama  ili  kupata nyadhifa mbalimbali.
Amesema Ofsi ya Waziri Mkuu Kuna miradi mingi ambayo inahusu Vijana hivyo Ni fursa kwake kufika kuweza kuona Ni namna gani atawasaidia huku akisema tayari Kuna nafasi milioni nane za ajira ambazo zimetengwa kwa ajili ya Vijana.

Na Barnabas kisengi Dodoma June 25 2021.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »