JAMII YATAKIWA KUSHIRIKI MAPAMBANO DHIDI YA UKATILI WA KIJINSIA

JAMII YATAKIWA KUSHIRIKI MAPAMBANO DHIDI YA UKATILI WA KIJINSIA

Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW Na Mwandishi Wetu, Dodoma  Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii imeitaka jamii ya kitanzania kushiriki kikamilifu katika mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia katika maeneo yao. Hayo yamebainika leo jijini Dodoma katika kikao kilichokutanisha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Mhe. Stansalus Nyongo akizungumza katika kikao kilichowakutanisha Kamati hiyo na Wizara ya Afya-Idara ya Maendeleo ya Jamii kuwapitisha katika mikakati ya Serikali ya kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia kilichofanyika jijini Dodoma.

Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Mhe. Neema Lungangira akitoa mchango wake wa nini kifanyike katika mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia katika kikao kilichokutanisha Kamati hiyo na Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii jijini Dodoma.

Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

 
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii imeitaka jamii ya kitanzania kushiriki kikamilifu katika mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia katika maeneo yao.
 
Hayo yamebainika leo jijini Dodoma katika kikao kilichokutanisha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii na Shirika la UNFPA kilicholenga kujadili jinsi ya kukomesha vitendo vya ukatili wa kijinsia katika jamii.
 
Akizungumza katika kikao hicho, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Stanslaus Nyongo amesema vitendo vya ukatili wa kijinsia vinatokea katika jamii na hivyo Jamii inawajibu wa kukomesha vitendo hivyo.
 
Ameongeza kuwa elimu inahitajika kwa kiasi kikubwa kwa jamii katika kuhakikisha inabadili mitazamo ambayo kwa kiasi kikubwa inasababisha vitendo vya ukatili wa kijinsia katika familia na jamii
 
“Tukifanikiwa kubadili mitazamo ya jamii zetu katika baadhi ya mambo hasi itasaidia sana kupungua kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia katika jamii zetu” alisema Mhe. Nyongo
 
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Godwin Mollel amesema kuwa Serikali inashirikiana na wadau mbalimbali likiwemo shirika la UNFPA katika kuhakikisha inawafikia jamii hasa za vijijini katika kuwapatia elimu katika midahalo na mikusanyiko  mbalimbali kuhusu madhara ya vitendo vya ukatili kwa ustawi wa jamii
 
Naibu Waziri Dkt. Mollel ameongeza kuwa vitendo vya ukatili wa kijinsia katika jamii zetu vinatokana malezi na makuzi ndani ya Jamii.


 

Raymond Ishengoma Mushumbusi

Information Officer Government Communication Unit
Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly and Children

+255715477877/+255789553222

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »