Bodi ya Baraza la Elimu Tanzania (TET) imetakiwa kufuatilia maoni ya wadau katika uboreshaji wa mitaala ya elimu nchini

Bodi ya Baraza la Elimu Tanzania (TET) imetakiwa kufuatilia  maoni ya wadau  katika uboreshaji wa mitaala ya elimu  nchini

Na Barnabas kisengi -Dodoma  SERIKALI imeagiza Bodi ya Baraza la Elimu Tanzania (TET) kuhakikisha inafuatilia maoni ya wadau kwa karibu ikiwemo kuyafanyia kazi ili yalete tija katika uboreshaji wa mitaala ya elimu ya awali,msingi na sekondari nchini ambayo itasaidia kuoa wahitimu wenye uwezo wa kujiajiri na kuajiriwa.Akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Wadau wa Elimu kuhusu

Na Barnabas kisengi -Dodoma 


SERIKALI imeagiza Bodi ya Baraza la Elimu Tanzania (TET) kuhakikisha inafuatilia maoni ya wadau kwa karibu ikiwemo kuyafanyia kazi ili yalete tija katika uboreshaji wa mitaala ya elimu ya awali,msingi na sekondari nchini ambayo itasaidia kuoa wahitimu wenye uwezo wa kujiajiri na kuajiriwa.
Akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Wadau wa Elimu kuhusu utoaji wa maoni ya uboreshaji Mitaala ya elimu ya msingi na sekondari,Naibu Waziri wa Elimu Omary Juma Kipanga amesema,Bodi hiyo inapaswa kuwa makini na maoni yanayochangiwa kwa sababu yanakwenda kuboresha mitaala ya elimu ya msingi.

Amesema kuwa serikali imeona kuwa itauwa ni vema kusitisha mabadiliko yoyote kwenye mitaala iliopo sasa na kuendelea na mtaala uliopo mpaka mchakato huu utakapokamilika.

“kama mtakumbuka kulikuwa na mchakato wa kuanzisha kufundisha somo la historia ambalo lingefundishwa kwa Kiswahili kuanzia ngazi ya chini ya awali na kuendelea hadi vyuo vikuu,lakini hivi sasa inasubiriwa mchakato huu ukamilike ili kupata mtaala Shirikishi na Jumuishi utakaowezesha wahitimu kujiajiri na kuajriwa”amesema kipanga

kutokana na kuanza kwa mchakato huu serikali imeona ni vema kuendelea na mtaala wa sasa,kama ilivyo ili kutoa fursa kwa wadau kutoa maoni yao ili kuwa na mtaala shirikishi na Jumuishi.

Aidha amefafanua zaidi ya kuwa katika karne ya 21 Dunia imeshuhudia mapinduzi makubwa ya Sayansi na Teknolojia yaliyoleta utawazi ambayo moja ya athari zake ni kuongeza ushindani katika soko la ajira,hivyo kuna umuhimu mkubwa wa kuhakikisha wahitimu wanapata ujuzi na maarifa utakaowawezesha kuwa na ufanisi katika soko la ajira ikiwemo kumudu maisha yao ya kila siku.

“Nchi yetu imejikita katika uchumi wa viwanda hivyo ni vema maoni yenu na masuala mengine yalenge kuweka msingi imara wa kuimarisha uchumi na uchumi wa viwanda hapa nchini”amesema kipanga
Mkutano huu ni muhimu sana kwa sababu utawezesha wadau kutoa maoni ya uboreshaji wa mitaala ngazi ya Elimu ya Msingi ili kuwezesha wahitimu kuwa na stadi za ujuzi unaohitajika katika jamii.

“mitaala bora ya ngazi hii itaweka misingi imara ya Elimu kwa ngazi zinazofuata ikiwemo kusababisha msingi huo kuwezesha wahitimu kuwa na maarifa na ujuzi stahiki na kuwajengea ari ya kupenda kujifunza zaidi ili kujenga mazingira wanayoishi na kufanya shughuli mbalimbali za kimaendeleo”amesema

Aidha amesema Rais kwa kutambua hili amesisitiza mara nyingi haja ya kuboresha mitaala inayotumika mashuleni.

Alifafanua zaidi ya kuwa washiriki wote wa kongamano hili washiriki kikamilifu kutoa maoni yenu ambayo yatafanyiwa uchambuzi wa kitaalamu kwa lengo la kupata mitaala bora itakayolenga kwenye ujenzi wa ujuzi kwa wahitimu.

Kipanga amesema hii sio mara ya kwanza kwa serikali kufanya maboresho ya Mitaala ya Elimu ya Msingi,kila kunapoonekana kuwa na sababu ya kufanya hivi, na hii imetokea mara kadhaa baada ya kuwa ana mabadiliko muhimu katika nchi n ahata kimataifa.

Amesema kuwa kuhakikisha kuwa mitaala inaendana na hali halisi ya Kijamii,kisiasa kiuchumi Sayansi na kiteknolojia ndani nan je ya nchi.

Hata hivyo kutokana na sababu hizo wamekuwa na mabadiliko ya Mitaala ya Elimu ya Msingi mara tano nah ii itakuwa ya Sita ambapo kila mabadiliko yalikuwa na matokeo yenye tija kulingana na umuhimu uliopo.

Bado kumekuwa na maoni kwamba elimu yetu haimpi muhitimu maarifa na ujuzi unaoendana na mahitaji ya sasa, kumekuwa na kilio ya kuwa wanahitaji kufanyike mjadala wa kitaifa ili kupata furasa ya kutoa maoni elimu na ujuzi watakaokuwa nao.

Dkt Lenadi  Akwilapo ni Katibu Mkuu Wizara ya Elimu amesema kuwa Uboreshaji wa mitaala ni jambo la muhimu kwani sana katika jamii na nchi yoyote kwani mar azote inalenga kuhakikisha kuwa elimu inayotolewa inakidhi mahitaji ya sasa na ya baadae kwa nchi husika.
Kama tunavyofahamu serikali ya awamu ya sita imeweka msisitizo ya kuhakikisha kuwa na wahitimu wenye ujuzi lengi ikiwa ni kukidhi mahitaji ya Tanzania ya uchumi wa kati na ujenzi wa Viwanda.


Akwilapo amesema sisi katika ngazi ya Wizara wapo tayari kusimamiazoezi hilo kuhakikisha kwamba linafanyika katika mafanikio makubwasana.
Naye Mwenyekiti wa TET Prof Bernadeta killian amesema wataendelea kuunga mkono jitihada za serikali katika kuhakikisha mitaala hiyo inatekelezwa ipasavyo ili kuongeza ufaulu Mzuri nchini.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »