Serikali itaendelea kuboresha mazingira ya Uwekezaji na Biashara nchini.

Serikali itaendelea kuboresha mazingira ya Uwekezaji na Biashara nchini.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC), leo tarehe 26 Juni, 2021 ameongoza Mkutano wa 12 wa Baraza hilo lililojadili mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na masuala ya kodi, Mamlaka za udhibiti pamoja mazao yatokanayo na misitu. Mhe. Rais Samia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Biashara Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akifungua Mkutano wa 12 wa Baraza la Taifa la Biashara katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete , Ikulu Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC), leo tarehe 26 Juni, 2021 ameongoza Mkutano wa 12 wa Baraza hilo lililojadili mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na masuala ya kodi, Mamlaka za udhibiti pamoja mazao yatokanayo na misitu. Mhe. Rais Samia amesema Serikali itaendelea kuboresha mazingira ya Uwekezaji na Biashara nchini ili kuchangia pato la Taifa. Amesema sekta binafsi ni mhimili muhimu wa maendeleo ya nchi kwasababu huchangia kwa kiasi kikubwa kukuza uchumi. Pia Mhe. Rais Samia amesisitiza kuwa hakuna Taifa lolote duniani ambalo linaweza kupiga hatua ya maendeleo bila kushirikiana na sekta binafsi. Mhe. Rais Samia amewaagiza Mawaziri wa sekta mbalimbali kukaa na kujadiliana na Wafanyabiashara wa sekta binafsi ili kuendelea kutatua changamoto zinazowakabili. Aidha, Mhe. Rais amewaagiza Wakuu wa Mikoa na Wilaya ambao ni Wenyeviti wa Mabaraza hayo katika ngazi za Mikoa na Wilaya kushirikiana na Sekretarieti ya Baraza Taifa na kuhakikisha Mabaraza hayo yanafanyika kwani ndio chimbuko la mabadiliko katika ngazi ya Taifa. Mhe. Rais Samia amesema Serikali imeamua kufufua mazungumzo ya utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo na mradi wa Mchuchuma na Liganga ili kuchochea kasi ya kukuza uchumi nchini. Amesema ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo ni muhimu kwasababu utaongeza uwezo wa kushindana na bandari shindani na kukuza uchumi wa Taifa. Kuhusu mikakati ya kuzisaidia sekta za utalii na usafiri wa anga ambazo zimeathiriwa na ugonjwa wa corona, Mhe. Rais Samia amesema Serikali imepunguza ada mbalimbali ikiwa ni pamoja na ada ya Wakala wa Wasafirisha Watalii kutoka Dola za Marekani 2,000 hadi Dola 500 kwa kampuni yenye magari kati ya 1 na 3. Kwa upande wake Mwenyekiti wa Sekta binafisi nchini (TPSF) Angelina Ngalula ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kujenga mazingira bora na rafiki kwa Wafanyabiashara na Wawekezaji kutokana na hatua mbalimbali zinazochukuliwa ikiwa ni pamoja na kufuta baadhi ya kodi na tozo ambazo zimesaidia kuimarisha biashara na uwekezaji nchini. Baraza la Biashara la Taifa (TNBC) limeanzishwa likiwa ni jukwaa rasmi la majadiliano kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi ili kuwezesha kupatikana kwa muafaka wa pamoja kuhusu masuala muhimu yanayohusu maboresho ya Sera, Sheria, Kanuni na Taratibu za biashara na uwekezaji nchini.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »