Wanafunzi 423 wa shule ya secondary pwaga wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma wanakaa chini.

Wanafunzi 423 wa shule ya secondary pwaga wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma wanakaa chini.

Wanafunzi 423 wa shule ya secondary pwaga wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma wanakaa chini kutokana na changamoto ya kutokuwepo na madawati ya kutosha shule hapo. Kutokana na jambo hilo la kutokuwa na madawati  ya kutosha shuleni hapo Kumemsukuma Mh Diwani wa Kata ya pwaga Willefred Mgonela kutafuta ufumbunzi wa changamoto hiyo ya madawati kwa kukutana na

Wanafunzi 423 wa shule ya secondary pwaga wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma wanakaa chini kutokana na changamoto ya kutokuwepo na madawati ya kutosha shule hapo.

Kutokana na jambo hilo la kutokuwa na madawati  ya kutosha shuleni hapo Kumemsukuma Mh Diwani wa Kata ya pwaga Willefred Mgonela kutafuta ufumbunzi wa changamoto hiyo ya madawati kwa kukutana na wananchi na kuwapatia elimu na kuweza kuchangia nguvu kazi na fedha na kuweza kutengeneza meza  na viti Mia moja ili kuweza kuwasaidia wanafunzi wasiendelee kukua chini katika kupata elimu shuleni hapo.

 
Awali akitoa taarifa ya shule ya secondary pwaga kwa Mh DIWANI wa Kata hiyo mkuu wa shule hiyo Mwalimu Nickson Tuya amesema shule ina jumla ya wanafunzi 1053 wakiwemo wanaume 489 wanawake 564 na ina jumla ya walimu 12 wakiwemo wanaume 12 wanawake 7 na wanaupungufu wa walimu 7 kwa sasa pia wanawalimu 2 ambao wanajitolea hawajaajiriwa na serikali.

 
Aidha mwalimu Tuya amesema jumla ya madawati yaliyopo ni 460 ambayo yanatumika na wanaupungufu wa madawati 591 ambayo yakipatikana yatakuwa yameondoa adha kwa wanafunzi waliopo shuleni hapo.


Diwani wa Kata ya Pwaga Willefredy Mgonela baada ya kupokea taarifa kutoka kwa mkuu wa shule hiyo akamweleza mkuu wa shule hiyo kuwa wamebahatika kupata meza na viti 170 ambavyo vitapunguza adha kwa wanafunzi shuleni hapo katika kipindi hichi ambapo wanafunzi wapo likizo hivyo wakifungu shule mwezi julai yataweza kuwasaidia baadhi ya wanafunzi huku akiendelea na mchakato wa kutafuta m engine. 


Aidha Diwani Mgonela amesema mchanganuo wa madawati hayo 170 ni ofisi ya mkulugenzi mtendaji wa halimashauri ya wilaya ya mpwapwa imewapatia meza na viti vyake 50, na ofisi ya mbunge wa Jimbo la kibakwe kwa kupitia fedha za mfuko wa Jimbo iliwapatia meza na viti vyake 20 huku wananchi wa Kata ya pwaga kwa kutumia nguvu zao na michango yao wameweza kutengeneza meza na viti vyake 100 hivyo kufanya kuwa na jumla ya meza na viti 170.


Diwani Mgonela amesema Tayari ameshakabidhi meza na viti hivyo kwa uongozi wa shule hiyo na kufanya sasa Wawe na idadi ya viti na meza 630 na bado wanaupungufu wa meza na viti 423 kutokana na idadi ya wanafunzi waliopo shuleni hapo.

 
Diwani willefredy mgonela amewataka wananchi na waduu wa Kata kuendelea kujitoa ili kuhakikisha meza na viti vilivyobaki 423 wanavikamilisha mapema na kupeleka shuleni hapo kwakuwa hakuna uridhi mzuri kwa watoto Kama elimu na hatajisikia vizuri akiwa madarakani wanafunzi wa Kata yake  kuendelea kukaa chini kwa kukosa viti na meza.

” hapa kwenye Kata yangu tunamsitu wa miti ya mbao tayari nimeshaomba kibali kwa mamlaka husika tumeruhusiwa kuvuna miti yetu hivyo naamini hadi kufikia mwezi agusti mwaka huu tutakamilisha meza na viti vyote ili kuhakikisha hakuna mwanafunzi kukaa chini tena maana swala la elimu ni kipaombele cha serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na RAIS MAMA YETU SAMIA SULUH HASSAN  lazima tumuenzi kwa vitendo sisi viongozi wa wananchi kwakuwa wametuchaguwa tuwatumikie” amesema mgonela. 

Na Barnabas kisengi Mpwapwa June 27 2021.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »