WAZIRI MKENDA AIPA RUNGU BODI YA WAKURUGENZI WA BODI YA KAHAWA//ONGOZENI KWA KUWA NA MAWAZO YA KIBIASHARA

WAZIRI MKENDA AIPA RUNGU  BODI YA WAKURUGENZI WA BODI YA KAHAWA//ONGOZENI KWA KUWA NA MAWAZO YA KIBIASHARA

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Moshi Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda ameitaka Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Kahawa ambayo ipo chini ya wizara ya kilimo kujiimarisha kiutendaji kwa ajili ya kufanya utafiti ili kuongeza tija ya uzalishaji wa kahawa. Waziri Mkenda ametoa maelekezo hayo tarehe 29 Juni 2021 wakati akizindua Bodi ya

Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda akisisitiza jambo wakati akizindua Bodi ya wakurugenzi wa Bodi ya Kahawa yenye makao makuu Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro tarehe 28 Juni 2021. 
Mwenyekiti wa Bodi Wakurugenzi wa Bodi ya Kahawa Prof. Aurelia K. N. Kamuzora akimkabidhi Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda zawadi ya Kahawa pamoja na begi mara baada ya kuzindua Bodi ya wakurugenzi wa Bodi ya Kahawa yenye makao makuu Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro tarehe 298Juni 2021.
Mwenyekiti wa Bodi Wakurugenzi wa Bodi ya Kahawa Prof. Aurelia K. N. Kamuzora akimkabidhi Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika Kahama (KACU) zawadi ya begi mara baada ya uzinduzi wa Bodi ya wakurugenzi wa Bodi ya Kahawa yenye makao makuu Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro tarehe 28 Juni 2021.
Mwenyekiti wa Bodi Wakurugenzi wa Bodi ya Kahawa Prof. Aurelia K. N. Kamuzora akisisitiza jambo mbele ya mgeni rasmi-Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda kwa ajili ya uzinduzi wa Bodi ya wakurugenzi wa Bodi ya Kahawa yenye makao makuu Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro tarehe 28 Juni 2021.

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Moshi

Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda ameitaka Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Kahawa ambayo ipo chini ya wizara ya kilimo kujiimarisha kiutendaji kwa ajili ya kufanya utafiti ili kuongeza tija ya uzalishaji wa kahawa.

Waziri Mkenda ametoa maelekezo hayo tarehe 29 Juni 2021 wakati akizindua Bodi ya wakurugenzi wa Bodi ya Kahawa Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro.Waziri Mkenda ameitaka Bodi hiyo kuhakikisha kuwa inaongoza sekta hiyo kwa kuwa na mawazo ya kibiashara ili kuwanufaisha wakulima na kuinufaisha nchi.

“Ninyi nyote mlioteuliwa wasifu wenu ndio muelekeo wetu, mnapaswa kufanya maamuzi mazuri kwani tunachotaka ni wakulima wetu kupata pesa za kukidhi mahitaji yao, mkifanya maamuzi ya kumuumiza mkulima yatakuwa hayatusaidiii” Amekaririwa Waziri Mkenda.

Kadhalika Waziri Mkenda ameitaka Bodi hiyo kutathmini wingi wa minada ya kahawa ambayo imegawanywa kwenye kanda kama ina tija kwa maendeleo ya zao la kahawa nchini.

“Mimi sijaja kuwashauri ninyi kwa kuwa ninyi ndio mmeteuliwa pia kwa ajili ya kunishauri mimi lakini hili la minada tazameni muone kama lina akisi matakwa ya biashara ya kahawa” Amekaririwa Prof Mkenda“Pia hakikisheni tunaimarisha uzalishaji na tija kwenye kahawa ili tuweze kuuza kwa bei nzuri na kuwashinda wengine, kwani namna pekee ya kushindana kwenye bei ni kuongeza tija”

Wajumbe walioteuliwa kuunda Bodi ya Kahawa inayoongozwa na Mwenyekiti wa Bodi hiyo Prof. Aurelia K. N. Kamuzora, ni Enock Chimagu Nyasebwa, Edson M. Rugaimukamu, Shadrack A. Issangya, Gotham Filipo Haule, Tinson Nzunda, Neel Vohora, Nangula H. Mwampamba, na Bahati Ludhabiho Mlwilo.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos

Translate »