Ajira Mpya zapunguza Tatizo la Walimu wa Physics na Mathematics

Ajira Mpya zapunguza Tatizo la Walimu wa Physics na Mathematics

Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI Mhe Uummy Mwalimu amesema kupitia ajira mpya za Walimu zilizotangazwa Tar 26.06.2021 hakuna shule yeyote itakayokuwa haina Mwalimu wa Physics wala Mathematics kwa kuwa wameajiriwa wa kutosha kupitia Ajira Mpya. Amesema Waalimu wa Physics walioajirwa ni 1,360 wakati shule ambazo hazikuwa na Mwalimu huyo ni 1,100 na Walimu

Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI

Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI Mhe Uummy Mwalimu amesema kupitia ajira mpya za Walimu zilizotangazwa Tar 26.06.2021 hakuna shule yeyote itakayokuwa haina Mwalimu wa Physics wala Mathematics kwa kuwa wameajiriwa wa kutosha kupitia Ajira Mpya.

Amesema Waalimu wa Physics walioajirwa ni 1,360 wakati shule ambazo hazikuwa na Mwalimu huyo ni 1,100 na Walimu wa Hesabu walioajiriwa ni 459 wenye Degree na 140 wenye Diploma wakati uhaba ulikuwa katika shule 400 hivyo kwa sasa shule zote zitakua na Walimu wa masomo hayo.

“Hivi karibu nikiwa Bungeni nilisema kuna shule wanafunzi wake hawajawahi kumuona Mwalimu wa Physics wala wa Mathematics na kwangu ile ilikua changamoto iliyopelekea kuhakikisha katika Ajira tulizotangaza tunatoa kipaumbele kwa Walimu wa masomo hayo nimefurahi sasa kuwa Walimu hao wamepatikana na watoto wetu sasa wanakwenda kusoma masomo hayo kwa uhakika zaidi” amsema.

Waziri Ummy ameyasema hayo alipotembelea shule ya Sekondari Bihawana katika Jiji la Dodoma kukagua maandalizi ya Mapokezi ya Kidato cha Tano ambao wataanza kuripoti shuleni kuanzia Tarehe 03-14/07/2021.

Jumla ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga ni Kidato cha Tano mwaka 2021 ni 87,663 ikiwa ni ongezeko la Wanafunzi 14,562 ukilinganisha na mwaka 2020 ambao walichaguliwa 73,101.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »