Serikali yatoa muongozo michango ya kujiunga na kidato cha tano

Serikali yatoa muongozo michango ya kujiunga na kidato cha tano

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Ummy Mwalimu amewaagiza wakuu wa shule wote nchini kuhakikisha michango ambayo wazazi wanatakiwa kutoa kwa ajili ya wanafunzi wanaojiunga na kidato cha tano kutokuzidi shilingi 188,000 ikiwemo na ada ya shilingi 70,000. Akiongea na waalimu leo alipotembelea shule ya Sekondari ya

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Ummy Mwalimu amewaagiza wakuu wa shule wote nchini kuhakikisha michango ambayo wazazi wanatakiwa kutoa kwa ajili ya wanafunzi wanaojiunga na kidato cha tano kutokuzidi shilingi 188,000 ikiwemo na ada ya shilingi 70,000.

Akiongea na waalimu leo alipotembelea shule ya Sekondari ya Bihawana kwa lengo la kuwaangalia maandalizi ya kuwapokea wanafunzi wa kidato cha tano Waziri Ummy amesema amesema mchango wowote kwa mwanafunzi anayeenda kuripoti kidato cha tano kwenye shule za Sekondari za Serikali hautakiwi kuzidi shilingi 188,000.

Waziri Ummy anafafanua kuwa Serikali imepokea malalamiko kutoka kwa Wazazi na Walezi kuwa Michango imekuwa mikubwa kiasi cha kupelekea wazazi au walezi wasio na uwezo kushindwa kujiunga na Kidato cha Tano, hivyo amewataka Wazazi kutokubali kulipa zaidi.

Amewaagiza Wakuu wa Mikoa , Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha wanasimamia maelekezo yaliyotolewa kwa kuzikagua kwa karibu Join instruction zinazotolewa na shule za Sekondari kwa ajili ya kujiridhisha na gharama iliyoelekezwa na Serikali.

Waziri Ummy amewaonya wakuu wa shule ambao watawatoza wazazi au walezi zaidi ya fedha zilizotolewa na Serikali hatasita kuwachukulia hatua za kinidhamu.

Vilevile, amewataka wazazi na walezi watakaofanya maamuzi ya kuwapeleka watoto wao katika shule binafsi kutoa taarifa kwa Serikali ili nafasi hizo ziweze kupangiwa wanafunzi wengine waliokosa nafasi

Waziri Ummy, ameziagiza Halmashauri zote nchini kuhakikisha wanafanya maandalizi ya kuwapokea wanafunzi wanaojiunga na Kidato cha Tano kwa mwaka 2021 ikiwemo usafi wa mazingira, chakula na mazingira ya kufundishia na kujifunzia.

Aidha amewataadharisha wazazi kuwa hadi kufikia Agosti 1, 2021 kama mwanafunzi hatakuwa ameripoti katika shule aliyopangiwa nafasi yake itachukuliwa na kupatiwa mwanafunzi mwingine.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »