TIGO KUTAMBULISHA SIMU MPYA YENYE OFA KABAMBE YA GB 96 MWAKA MZIMA

TIGO KUTAMBULISHA SIMU MPYA YENYE OFA KABAMBE YA GB 96 MWAKA MZIMA

Leo Julai 2, 2021 Kampuni namba moja ya Huduma za Kidigitali hapa nchini Tigo Tanzania imetambulisha rasmi Ubia na Kampuni inayotengeneza, Kusambaza na Kuuza Simu Janja hapa nchini Xiaomi kwa mara ya kwanza kabisa, ambapo siku ya Leo Rasmi Xiaomi inawaletea Watanzania Redmi 9T simu yenye ubora wa Hali ya Juu na Inakuja Na Ofa

Leo Julai 2, 2021 Kampuni namba moja ya Huduma za Kidigitali hapa nchini Tigo Tanzania imetambulisha rasmi Ubia na Kampuni inayotengeneza, Kusambaza na Kuuza Simu Janja hapa nchini Xiaomi kwa mara ya kwanza kabisa, ambapo siku ya Leo Rasmi Xiaomi inawaletea Watanzania Redmi 9T simu yenye ubora wa Hali ya Juu na Inakuja Na Ofa kabambe ikiwemo GB 96 za Intaneti Bure kwa Mwaka Mzima.

Akizungumza wakati wa Kutambulisha Ubia huo Meneja wa Bidhaa za Intaneti Kutoka Tigo Bwana Mkumbo Myonga amewaomba Watanzania waweze kufika Kwenye banda la Tigo lililopo kwenye maonyesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar Es Salaam (Sabasaba) na maduka mbalimbali ya Tigo hapa nchini kwa ajili ya kujipatia simu hiyo kwa bei nafuu ikiwa Na Ofa Kibao.

Kwa Upande Wake Meneja Masoko Msaidizi wa Kampuni ya Simu ya Xiaomi Bwana Katembo Ibrahim amewasihi watanzania kuichangamkia Redmi 9T kwa maana ni simu Janja ya Kisasa yenye Ukubwa wa Kioo 6.53 , Camera ya Nyuma Megapixels 48 na 8 megapixels Camera ya mbele kwa ajili ya Selfie bora zaidi, Storage GB 128 pamoja na 4 GB RAM, Uwezo Mkubwa wa betri yenye uwezo wa 6000 Mih na sifa nyingine kibao.

“Nawakaribisheni wateja wetu kwenye viwanja vya Sabasaba na maduka ya Tigo Kwa ajili ya kujipatia Simu yetu ya Redmi 9T na kufuatilia ukurasa wetu wa Instagram ambao ni xiaomi_tanzaniaofficial” Aliongezea Bwana Ibrahim

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »