SERIKALI YAWAITA KAZINI WATUMISHI 473 KADA YA AFYA KATIKA NAFASI MBALIMBALI.

SERIKALI YAWAITA KAZINI WATUMISHI 473 KADA YA AFYA KATIKA NAFASI MBALIMBALI.

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya imewaita kazini watumishi wa Umma katika kada ya Afya  wapatao 473 wakiwemo Madaktari Bingwa,Wauguzi na Wataalam wa mionzi waliokidhi vigezo vya ajira. Hayo yameelezwa leo Jijini Dodoma na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Profesa Abel Makubi wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na ajira hizo. Profesa Makubi amesema watumishi

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Profesa Abel Makubi.

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya imewaita kazini watumishi wa Umma katika kada ya Afya  wapatao 473 wakiwemo Madaktari Bingwa,Wauguzi na Wataalam wa mionzi waliokidhi vigezo vya ajira.

Hayo yameelezwa leo Jijini Dodoma na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Profesa Abel Makubi wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na ajira hizo.

Profesa Makubi amesema watumishi hao waliochaguliwa ni kutokana na kujaza nafasi zilizoachwa wazi na watumishi wa kada mbalimbali katika Sekta hiyo ambao walifikia ukomo wa utumishi ikiwemo  kustaafu,kufariki na wengine kuacha kazi.

Hata hivyo amefafanua kuwa jumla ya nafasi 473 zilitangazwa na Wizara ya Afya kupitia tovuti ya Wizara mnamo Mwezi mei mwaka huu na walipokea jumla ya maobi 19757 kati ya hayo maombi4760hawakukamilisha kujaza maombi yao na hivyo kutokidhi vigezo huku maombi9338 yakiwa yamekidhi vigezo vya kuajiriwa.

Katika hatua nyingine Katibu Mkuu huyo amewataka waliochaguliwa katika nafasi hizo kuripoti katika Hospitali ya Mirembe Jijini Dodoma kuanzia leo hadi Julai9 Mwaka huu wakiwa na nakala halisi pamoja na vivuli vya vyeti yao.

Pia Katibu Mkuu huyo ametoa wito kwa waombaji wote wa nafasi za ajira kuhakikisha wanakuwa makini katika kujaza fomu za maombi ya kazi ili kukidhi vigezo.

Na Barnabas kisengi Dodoma Julai  05 2021

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »