Kata ya chamkoroma imetekeleza maagizo ya serikali ya kuanzisha kilimo cha bustani za mbogamboga katika shule zote 7 za msingi na secondary .

Kata ya chamkoroma imetekeleza maagizo ya serikali ya kuanzisha kilimo cha bustani za mbogamboga katika shule zote 7 za msingi na secondary .

Katika kutekeleza maagizo ya serikali ya Lishe endelevu kwa shule za msingi na secondary yaliyotolewa na waziri mkuu kukabiliana udumavu na utapiamlo kwa wanafunzi na watoto wilayani kongwa katika Kata ya chamkoroma wamefanikiwa kutekeleza maagizo hayo ya serikali kwa kuanzisha kilimo cha bustani za mbogamboga katika shule zote 7 za msingi na secondary moja. Akiongea

Afisa Elimu Kata ya Chamkoloma Mwalimu Sifrasi Japheth Nyakupola.


Katika kutekeleza maagizo ya serikali ya Lishe endelevu kwa shule za msingi na secondary yaliyotolewa na waziri mkuu kukabiliana udumavu na utapiamlo kwa wanafunzi na watoto wilayani kongwa katika Kata ya chamkoroma wamefanikiwa kutekeleza maagizo hayo ya serikali kwa kuanzisha kilimo cha bustani za mbogamboga katika shule zote 7 za msingi na secondary moja.


Akiongea na Jfive tv oneline Afisa Elimu Kata ya Chamkoloma Mwalimu Sifrasi Japheth Nyakupola amesema ametekeleza maagizo hayo ya serikali kwa vitendo kwa kuanzisha bustani darasa katika shule zote za msingi na secondary katika Kata ya chamkoroma.


Mwalimu Nyakupola amesema kuanzishwa kwa bustani darasa katika shule 7 za Kata yake kumewawezesha wanafunzi kujifunza kulima mbogamboga na pia kuweza kupata mboga katika chakula cha mchana ambacho wanafunzi wanakula shuleni hapo na kuendelea na vipindi .


Aidha Mwalimu Nyakupola amewataka wanafunzi kuhakikisha kila wanapo patiwa chakula cha mchana shuleni hapo wahakikishe wanapatiwa na mboga za majani kwakuwa wanazizalisha wao wenyewe katika maeneo ya mashamba ya shule.


“Licha ya mboga hizi kuliwa na wanafunzi bado umekuwa ni mradi wa shule kwakuwa pia tunaziuza kwa wananchi wa maeneo ya jirani na shule  na kuweza kuleta kipato katika shule na kwa sasa tumeamua kuanzisha bustani darasa katika Shule yetu ya secondary ya  Mag’hweta ili nao wanafunzi hao waweze kujifunza kulima bustani ya mbogamboga”amesema Nyakupola.


Aidha Mwalimu Nyakupola amezitaja shule hizo zinazojihusisha na kilimo cha bustani ya mbogamboga kwa shule za msingi ni chamkoroma, makole,  Tubugwe,  Mag’hweta, Tubugwe kibaoni, mseta bondeni na kwa sasa wameanzisha kilimo hicho kwa shule ya sekondary Mag’hweta ambayo ni secondary ya kata.


Afisa Elimu Kata hiyo amewaomba maafisa elimu Kata wenzake wa Kata zote za wilaya ya kongwa nao kuanzisha bustani ya mbogamboga katika maeneo yao kutokana na hali ya hewa ya maeneo yao walipo katika Kata zao. .

Na Barnabas kisengi KongwaJulai  06  2021.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »