Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Antony Mtaka amewataka Maafisa Ardhi kutumia kauli nzuri wanapotoa huduma kwa wananchi.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Antony Mtaka amewataka Maafisa Ardhi kutumia kauli nzuri wanapotoa huduma kwa wananchi.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Antony Mtaka amewataka Maafisa Ardhi kutumia kauli nzuri pindi wanapotoa huduma kwa wananchi. Mtaka ameyasema hayo  jijini Dodoma,ikiwa ni muendelezo wa kampeni  ya siku kumi (10) ya kutatua migogoro ya Ardhi jijini hapa. Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Dkt. Fatuma Maganga amewataka wananchi kutumia siku kumi vizuri kupeleka

Mkoa wa Dodoma Antony Mtaka.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Antony Mtaka amewataka Maafisa Ardhi kutumia kauli nzuri pindi wanapotoa huduma kwa wananchi.

Mtaka ameyasema hayo  jijini Dodoma,ikiwa ni muendelezo wa kampeni  ya siku kumi (10) ya kutatua migogoro ya Ardhi jijini hapa.

Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Dkt. Fatuma Maganga amewataka wananchi kutumia siku kumi vizuri kupeleka malalamiko ya migogoro wanayokumbana nayo katika maeneo yao huku akiwapongeza waliofika kwakuwa hapo ni sehemu sahihi ya kutatua migogoro hiyo.

Awali wakizungumza mbele ya Mkuu huyo wa Mkoa wananchi walioshiriki katika zoezi hilo la utatuzi wa migogoro ya ardhi katika ukumbi wa Jakaya Kikwete akiwemo Alpha George  amesema anaamini kuwa matatizo hayo yatashughulikiwa huku Regina Bilingi wa Makulu akisema walikuwa na mashamba tambukareli ambapo kwa sasa panaitwa medeli hawajapewa fidia yeyote tangu walipohamishwa.

Naye  Bwana Godffrey ameelezea changamoto ya eneo ambalo limetwaliwa na jiji huku akisema ni matumaini yake kuwa mgogoro huo utashughulikiwa huku Elizabelth Mwakasaka wa Mkoa wa Njombe akieleza kwa uchungu mkubwa anasema yeye ni mama wa watoto wa nne na ni mjane changamoto yake kubwa ni eneo lake kupewa mtu mwingine na pindi anapodai eneo hilo imekuwa ni ngumu kulipata.

Wananchi

Kampeni hiyo ya utatuzi wa migogoro ya ardhi jijini Dodoma ilianza jana  ambapo kwa siku tatu timu ya wataalamu  itakuwa  katika ukumbi wa JK na kisha kwa siku 7 wataenda katika Kata 41  ili kuitatua migogoro hiyo kwa vitendo.

Na Barnabas kisengi Dodoma.Julai   6 2021.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Translate »